Kamanda Muslim amewataka
madereva kuwa waangalifu katika kuhakikisha usalama wa abiria hasa
katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutikana na uzoefu wa huko nyuma
kwamba kipindi kama hiki hutokea ajali nyingi.
Muslim pia aliwataka
madereva kuzingatia suala la afya na kuwasisitiza kutosimamisha magari
sehemu zisizo rasmi kwaajili ya abiria kujisaidia, amesema suala hilo
maarufu kama kuchimba dawa ni kosa kisheria na sio salama kwa wananchi
kujisaidia vichakani na wanaweza pia kuwasababishia ajali kutokana na
madereva kusimamisha magari maeneo ambayo sio salama, badala yake
amewataka kusimamisha magari maeneo ambayo yamejengwa vyoo na
yameandaliwa rasmi kwa abiria kupata huduma hiyo. (Picha na Habari na Jeshi la Polisi).
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Fortunatus Muslim, akizungumza na
madereva wa mabasi yanayokwenda mikoani.
No comments:
Post a Comment