HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2019

MAZINGIRA SI RAFIKI KWA WANAWAKE

Na Mauwa Mussa

Naibu Kiongozi wa Ngome ya Wanawake wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zahra Ali Hamadi amesema mazingira si rafiki ya  kuwashawishi wanawake wasomi kugombea nafasi za uongozi katika vyama vya siasa.

Ameyasema hayo wakati wa mahojianao na tasisi zisizo za kiserikali ambazo zinafanya utafiti wa kujua changamoto zinazowakwamisha wanawake katika vyama vya siasa kugombea nafasi za uongozi hapo ofisi ya chama  cha ACT Wazalendo iliyopo Vuga Mjini Zanzibar. 

Alisema pamoja na kuwa serikali imeruhusu mfumo wa vyama vingi lakini bado inawakwaza wanawake kwani mazingira  hayajawa rafiki kuwashawishi wanamke kugombea nafasi ya uongozi kutokana Serikali iliyopo madarakani kukandamiza vyama hasa vya upinzani na vitisho kwa viongozi wake.

Alifahamisha kuwa ili wanawake waingie kwa wingi katika nafasi za uongozi serikali inatakiwa iweke mazingira mazuri na hali bora ya demokrasia.

Alisema wanawake wengi hasa wasomi wanashindwa kuingia katika harakati za siasa kutokana na kuhofia usalama wao hasa wakati wa uchaguzi.

Pia alifahamisha kuwa kuwepo kwa mifumo dume katika vyama vya siasa pamoja na mila na tamaduni  ni miongoni mwa changamoto zinazowanyima fursa wanawake kugombea nafasi hizo.

Hata hivyo alisema kwa mwaka 2020 wanamatarajio makubwa ya wanawake wa chama hicho kugombea nafasi za uongozi kwani wamejipanga mapema ili kuingia katika uchaguzi.

Nae naibu katibu mkuu wa chama hicho nd Hamad  Mussa alisema ili wanawake waweze kushawishika na kuingia katika nafasi za uongozi ni lazma serikali iweke mazingira mazuri wakati wa uchaguzi.

“Wanawake wanakabiliwa na changamoto ya hali ya kiuchumi na kukosa utayari ambapo wengi wao hushindwa kumudu kugombea nafasi za uongozi.”alisema Naibu Hamadi Mussa.

Hata hivyo alisema katika chama chake ambacho kina asilimia kubwa ya viongozi wanawake akiwemo katibu mkuu wa chama hicho ndugu Dorathon ambae ni mwanamke.

Sambamba na hilo naibu huyo alisema chama chake kimengeza mtandao katika maeneo mbali mbali na kutoa fursa kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi.

Kwa upande wake muawakilishi kutoka asasi za kiraia kutoka Zanzibar Gender Coalition Bi Asha Abdu amewataka viongozi wa vyama vya siasa kufanya ushawishi kwa wanawake wa vyama hivyo ili kugombea nafasi za uongozi.

Bi Asha amesema wanawake wa vyama vya siasa wameonekana kuwa wachache katika nafasi za uongozi hasa katika vyombo vya kutunga sheria.

Asasi zisizo za kiserikali ikiwemo chama cha wandishi wa habari wanAwake  TAMWA zinafanya utafiti katika vyama vya siasa ili  kujua changamoto zinazowakabili wanawake katika kugombea nafasi za uongozi.

No comments:

Post a Comment

Pages