December 19, 2019

MKOA WA MOROGORO YAPATA CHANZO CHA UHAKIKA WA MAJI

 Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kuangalia chanzo cha maji cha Milima ya  Ulugulu katika eneo la Hululu ambapo mitambo itajengwa kwa ajili ya kusambaza maji katika mkoa wa Morogoro.
 Mhandisi wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana na umuhimu chanzo cha maji cha uhakika  kwa mkoa wa Morogoro  wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji Juma Oweso  ya kwenda kuangalia chanzo hicho cha maji.
 Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso, akipumuzika  na viongozi mbalimbali wakati kupanda mlima wa kufikia chanzo cha maji katika eneo Hululu.
 Sehemu ya chanzo ambapo mtambo utajengwa kwa ajili ya maji katika mkoa wa Morogoro.


Na Mwandishi Wetu

MKOA wa Morogoro hivi karibuni itaondokana na tatizo  la maji kutokana na kupata chanzo cha uhakika kutoka milima ya Ulugulu katika eneo la Hululu ambapo bwawa la Mindu litatumika kama ziada ya Maji.
Chanzo cha maji hicho kimefikiwa na Naibu Waziri wa Maji Juma  Aweso wakati alipokwenda kuangalia chanzo hizo na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu  pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira (Moruwasa).
Katika ziara ya Naibu Waziri Oweso aliwaagiza na Watendaji wa Bonde la Wami/Ruvu  pamoja na Mamlaka ya Safi na Mazingira (Moruwasa) kuandika andiko kwa kina ili kuwekeza miundombinu katika chanzo cha maji cha milima Ulugulu katika eneo la Hululu.
Viongozi wa eneo la chanzo cha maji walieleza kuwa Naibu wa Waziri huyo ni kiongozi wa kwanza kufika eneo la chanzo cha maji tangu dunia iiumbwe na kudai kuwa serikali ya awamu ya Tano ina udhubutu wa viongozi katika utendaji wa kuhakikisa wananchi wa Mkoa wa Morogoro wanaondokana na tatizo la maji.
Naibu Waziri Aweso  amesema kuwa kutokana na chanzo cha maji hayo kuwepo kwa muda wote kulikuwa hakuna sababu ya kutumia Bwawa kwani mabwawa huwekwa  sehemu ambayo ni kame hivyo mkoa wa Morogoro si Kame kwa kuwa na chanzo cha maji kinachotegemea  bwawa.
Amesema kuwa chanzo hicho cha maji katika milima ya Ulugulu ni kufikisha Morogoro ni jirani ukilinganisha na mradi wa maji wa Ziwa Victoria kutolewa mwanza na kwenda katika mikoa mbalimbali ambayo ilikuwa na ukame wa maji na hawakujua watapata katika chanzo kipi.
Nae Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu  Mhandisi Simon Ngonyani alimweleza kuwa chanzo hicho kinatokana na utunzwaji wa mazingira na kutaka wananchi waendelee kulinda vyanzo vya maji.
Ngonyani amesema kuwa kuna miradi mbalimbali ya miundombinu katika Mkoa wa Morogoro lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na kwenda kwa kasi katika ujenzi wa viwanda ambavyo kuendelea kwake kunatokana na upatikanaji wa maji.
Mhandisi Ngonyani amesema kuwa wanapokea maagizo ya Naibu Waziri  Juma Aweso na kuahidi watafanyia kazi kwa kuandika andiko la mradi kwa kushirikiana na Moruwasa ikiwa chanzo hicho kuanza kufanyiwa kazi.
“Ninaamini chanzo hiki kitakuwa mkombozi kwa wananchi wa  Mkoa wa Morogoro  na kuwa historia kutegemea bwawa kwa mkoa wenye vyanzo vya maji Lukuki  hivyo bonde litaendelea kuhakikisga vyanzo vya maji vinalindwa vizazi kwa vizazi”amesma Ngonyani.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero  Mwalimu Mohamed Utaly  amesema kuwa chanzo cha maji  hicho kwa Mkoa wa Morogoro kwa serikali ya awamu  chanzo cha maji kitajengwa. 

No comments:

Post a Comment

Pages