December 19, 2019

WATU WATATU WAFA WAKICHIMBA MADINI

Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la watu watatu kufariki baada ya kukosa hewa wakati wakichimba madini aina ya tini. (Picha na Lydia Lugakila, Kagera).
 Muonekano wa shimo waliloingia wachimbaji hao na kupoteza maisha baada ya kukosa hewa safi.
 Waokoaji wakitafuta miili ya waliofariki.



Na Lydia Lugakila, Kagera

Raia watatu toka nchini Burundi wamefariki dunia wakati wakiendelea na shughuli ya uchimbaji madini baada ya kukosa hewa safi katika shimo lenye urefu wa mita 35 wilayani Ngara mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele, amesema watu hao waliojulikana kuwa raia wa nchi jirani ya Burundi wamefariki dunia baada ya kukosa hewa safi katika shimo lenye urefu wa mita 35 wakati wakiwa katika uchimbaji wa madini.

Kufuatia tukio hilo lililotokea k
atika Kijiji cha Kihinga wilayani Ngara mkoani hapa serikali imepiga marufuku uchimbaji na kufunga kwa muda mgodi wa machimbo ya madini aina ya tini uliopo kijiji cha Kihiga kata ya kibogora wilaya humo.

Kufuatia watu hao kufariki kwenye machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani hapa amesema serikali imepoteza nguvu kazi ya Taifa na kwamba watu wote waliokuwa wakijishughulisha kwenye machimbo hayo wanatakiwa kuondoka na kuitaka wizara ya madini kufuatilia uwepo wa mgodi huo.

Amesema ikiwa agizo hilo litapuuzwa serikali ya kijiji cha kihinga watachukuliwa hatua na kuvitaka vyombo vya dola kumsaka mmiliki wa shimo hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages