Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw.
Gabriel Daqaro akiangalia bidhaa aina ya
mvinyo unaotengenezwa na Bi. Magreth Ibrahim wa Joma Enterprises kabla ya
kufunga Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini Arusha.
Na
Mwandishi Wetu, Arusha
Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Bw. Gabriel Daqaro amewataka wanawake wajasiliamali Mkoani Arusha kuwa wazalendo
kwa kulipa kodi pale biashara yao inapokuwa kubwa kwa kuwa jukumu la
kujenga Nchi ni la kwetu sote akionya kuwa baadhi ya watu wasidhani hawana
jukumu la kujenga Nchi.
Pamoja na mambo
mengine Bw. Daqaro amewataka wanawake wajasiliamali hao kutumia fursa waliyopata
ya elimu ya ujasiliamali kuwasaidia kuwekeza ili waweze kubadilisha maisha yao,
familia na Taifa kwa ujumla.
Bw. Daqaro Ameyasema
hayo wakati wa hotuba yake yakufunga Kongamano la Siku mbili la uwezeshaji
wanawake kiuchumi waliokusanyika kutoka Wilaya za Mkoa wa Arusha na kuongezewa
ujuzi kwa kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali.
Aidha Bw. Daqaro
amewataka Wajasiliamali hao kurasimisha biashara ili waweze kuwa katika mfumo
unaojulikana unaotambulika na serikali ili wote tushirikiane kujenga Taifa letu
na kuwataka kutambua kuwa inabidi kushirikiana na serikali kujenga Nchi hii.
Bw. Daqaro amewataka
wajiasiliamali hao wanawake kuzingatia viwango vya ubora katika bidhaa zao ili
ziweze kushindana katika soko kwa kuhakikisha wanakuwa na vifungashio imara na
bora ili bidhaa zao ziweze kukidhi ubora na kushindana katika soko.
Amelitaka Shirika la
Viwanda vidogo Nchini SIDO kuendelea kutoa elimu ya biashara kwa vikundi vya
akina mama ili viweze kuzalisha bidhaa bora zinazoweza kushindana katika Soko.
Akiongea wakati wa
kufunga Kongamano hilo Bi. Mboni Mgaza
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Wanawake kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii amesema washiriki wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake kiuchumi
walifikia 200 na wamepatiwa mafunzo mbalimbali ua ujasiliamali pamoja na
uzalishaji bidhaa kwa lengo la kukuza uwezo wao wa kiuchumi.
Bi. Mboni Mgaza pia
wanawake kupitia Kongamano hilo wameweza kuonesha na kuuza bidhaa zao lakini
pia kuna baadhi ya wanawake ambao wamepatiwa mafunzo na Taasisi mbalimbali
ambazo zilitoa jumla ya mada 13.
Naye Mshiriki wa Kongamano
hilo Bi. Irene Paranjo amesema Kongamano hilo limeleta faida kwa wanawake hao
kwani wameweza kujenga mtandao lakini pia kubadilishana Mawazo ya namna ya
kuboresha biashara zao lakini pia imekuwa ni fursa kwao kukutana na viongozi wa
juu ambao wamehaidi kuwasaidia katika juhudi za Serikali za kuwezesha wanawake
kiuchumi.
Serikali imekuwa
ikitoa Mikopo kupitia Serikali za Mitaa kwa Wanawake waliokatika vikundi vya
hisa na ujasiliamali kwa lengo kuwezesha wanawake kiuchumi na tayari Serikali
tayari kupitia mapato ya Halmashauri zote Ncini inatenga asilimia kumi ya
mapato yake kwa lengo la kuwezesha wanawake vijana na walemavu.
No comments:
Post a Comment