HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2019

NGARA YAONGOZA MIMBA ZA MASHULENI


Msichana mjamzito. (Picha na VOA).


Na Lydia Lugakila, Bukoba

Wanafunzi 65 wa shule za msingi na Sekondari kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Kagera wamepata mimba kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu.

Takwimu hizo zimetolewa na Afisa Elimu Mkoa wa Kagera, Juma Mhina, wakati akitoa taarifa ya hali ya elimu kwa mkoa huo katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika Manispaa ya Bukoba.

Mhina amesema takwimu hizo zimepungua kutoka wanafunzi 201 waliopata mimba mwaka 2018 hadi kufikia wanafunzi 65 hadi Novemba 2019 sawa na asilimia 68.

Amesema watuhumiwa waliohusika na vitendo hivyo wamefikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea kusikilizwa.

Ameongeza kuwa katika takwimu hizo halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani hapa imeongoza kwa mimba 16 manispaa ya Bukoba mimba 14 wilaya ya Muleba mimba 13 wilaya ya Misenyi mimba 9 Halmashauri ya Bukoba mimba 11 wilaya ya Karagwe mimba 2 na wilaya ya Kyerwa mimba 2.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameeleza kuwa ili kukomesha tatizo la mimba kwa wanafunzi jamii inatakiwa kushirikiana na Serikali kutoa taarifa za wahusika wa mimba hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages