December 06, 2019

SBL yaja na punguzo la bei

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti, akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo.
 Meneja Afya na Usalama Mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), David Mwakalobo (kulia), akifafanua jambo kwa baadhi wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari waliotembelea kiwanda cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo. 


Na Suleiman Msuya

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL), imetangaza punguzo la bei ya vinywaji vikali kwa watumiaji wa vinjwaji hivyo katika msimu wa sikukuu.

Tangazo hilo limetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, wakati akizungumza na waandishi wa habari walitembelea kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Chang'ombe wilayani Temeke jijijini Dar es Salaam.

Alisema watumiaji wa pombe kali zinazozalishwa na kusambazwa na SBL wanaombwa kutumia fursa hiyo ya punguzo kupata vinywaji hivyo.

Ocitti alisema punguzo hilo linaonesha namna SBL inavyowajali wateja wake hasa kipindi hiki cha sikukuu.

"SBL imepunguza bei ya vinywaji vikali ili kuwawezesha wateja wetu kununulia ndugu jamaa na marafiki zawadi za vinywaji ubora wa kimataifa kwenye sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya," alisema.

Mkurugenzi huyo alitaja vinywaji vitakavyohusika na punguzo hilo ni Johnnie Walker, Captain Morgan, Ciroc, Smirnofy Vodka na nyingine.

"Kampeni hii imeenda sambamba na wito wetu wa kunywa kistaarabu ambapo tunawaelimisha wateja wetu kuepuka kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto," alisema Ocitti.

Alisema kampeni ya endesha kistaarabu imekuwa ikifanyika kila mwaka ambapo kwa sasa ni mwaka wa tano kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine.

Mkurugenzi huyo alisema kampeni kunywa kistaarabu imelenga kuwepo kwa wateja endelevu wa bidhaa zao.

Kuhusu upanuzi wa viwanda na mwenendo wa kibiashara alisema kwa sasa wanatarajia kutumia Paundi Milioni 14 kupanua kiwanda cha Dar es Salaam.

Ocitti alisema baada ya upanuzi huo kukamilika wanatarajia kuongeza uzalishaji kwa asilimia 34 pamoja na ajira kwa Watanzania.

"Upanuzi tunaofanya unaonesha nia yetu ya kupanuka na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zetu pamoja na kutengeneza ajira zaidi. Pia utaongeza mahitaji ya malighafi tunazonunua kutoka kwa wakulima wa ndani kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu," alisema.

Alisema SBL inanua tani 17,000 za mahindi na uwele kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilomia 70 ya jumla ya mahitaji yote ya malighafi kwa mwaka.

Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa SBL imelipa Sh.Bilioni 120 kama l kodi mbalimbali za Serikali.

No comments:

Post a Comment

Pages