Na Mwandishi Wetu
MADEREVA zaidi ya 200 wa Jijini Mbeya
wamejiunga katika mfumo wa Mtandao wa Kimataifa unaotoa huduma za usafiri (inDriver).
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ...ilisema kuwa Mtandao huo wa
kimataifa unatoa huduma za usafiri wenye makao makuu yake Mountain
View-California, Marekani na unatumiwa na watu zaidi ya milioni 35
kupitia miji zaidi ya 30.
"Mbeya
ni jiji la pili kuzindua mfumo huu wa usafirishaji wa inDriver, baada
ya Arusha. Ambapo umeweza kuunganisha zaidi ya madereva 200 wa mjini
Mbeya, na wengine wengi wanaendelea kusajiliwa kila siku. Katika hatua
za awali,mfumo huu wa inDriver hautatoza madereva kiasi chochote cha
kamisheni," Ilifafanua.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, watumiaji wa mtandao huo wanaweza kupanga bei
ya usafiri kwa uhuru wakati madereva wanaweza kuchagua njia (route)
zenye faida na wanazozipendelea wao wenyewe.
Ilisema
kuwa Mfumo wa program hiyo unazuia kuongezeka kwa gharama kama vile
kukiwa na foleni, na historia ya maombi ya safari kitu ambacho ni
tofauti na makampuni mengine ambayo yanaongeza bei.
"Mfumo
huu wa usafirishaji unaruhusu abiria kuweka nauli zao wenyewe kwa njia
watakayoichagua na kuipendelea. Madereva wa karibu ambao wanapata
taarifa ya kupata usafiri huwa wana chaguzi tatu," ilieleza taarifa hiyo
Taarifa
hiyo ilizitaja chaguzi hizo kwa madereva ni kukubali nauli inayotolewa,
kupuuza nauli inayotolewa au kufanya mazungumzo ili nauli iongezeke.
Ilisema kuwa abiria anaweza kuchagua aina ya gari anayohitaji au bajaji.
Taarifa
aliongeza kuwa kitu pekee cha tofauti katika mfumo huu wa inDriver ni
kwamba madereva hawajasajiliwa moja kwa moja (automatically) kwa
watumiaji.
"Abiria
anachagua dereva atakayeona anafaa zaidi na aina ya vipaumbele vyenye
umuhimu kwake binafsi kama vile gharama za nauli, kiwango cha dereva,
makadirio ya muda wa kuwasili na aina ya gari litakalotumika.
Iliongeza
kuwa mfumo huo wa inDriver una chaguo la kumfanya mtumiaji asafiri
salama huku abiria anaweza akatumia GPS (mfumo wa kuonesha mahala mtu
alipo) ya maeneo ya safari kwa wakati halisi kutoka kwenye programu kwa
mawasiliano kwa watu wanaoaminika.
"Kusafiri
na inDriver kunaweza kufanyika kupitia mipaka ya jiji la Mbeya na
vitongoji vya karibu.Kwa sasa, malipo yanaweza kufanyika hapo kwa hapo,
pia inaruhusu kupunguza gharama za safari, kama malipo yakifanyika
kupitia kadi kutakuwa na makato kiasi," ilieleza
Taarifa hiyo ilisema kuwa, abiria anaweza kuupakua mfumo huu wa inDriver bure kutoka Google Play Store and AppStore.
No comments:
Post a Comment