Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe ametoa msimamo huo wa Serikali
alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio katika ofisi ndogo
za Wizara jijini Dar es Salaam
Aidha, Dkt. Mnyepe ameitaka UNHCR kuzingatia na kuheshimu
makubaliano baina yake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1991
hususani Ibara ya Pili na ya Tatu (Articles II & III). Ibara hizo
zinaelekeza kwamba UNHCR ni lazima ishirikiane na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kutekeleza majukumu yake hapa Nchini.
Hivi karibuni UNHCR ililitaka Shirika la Msalaba mwekendu
Tanzania (TRCS) kukabidhi majukumu yao bila kuihusisha serikali. Hatua hiyo ya
UNHCR inavunja makubaliano ya 1991.
Hivyo amewaeleza UNHCR kwamba Shirika la Msalaba mwekundu Tanzania
kuendelea na majukumu yake kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo mpaka Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na UNHCR watakapokubaliana vinginevyo.
Naibu Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George
Kuchio (kushoto) akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe wakati wa mazungumzo katika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe (kulia) akimueleza jambo Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. George Kuchio. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment