December 24, 2019

Jamii yatakiwa kubadilika na kutumia teknolojia ya kisasa

Na Mwandishi Wetu

JAMII nchini imetakiwa kubadilika na kutumia tekonojia za kisasa ambazo zitachagiza ukuaji wa uchumi.

Akizungumza na waandishi wa Habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa wanafunzi wa Chuo cha Elimu  ya Biashara (CBE), wanaosoma mizani Mwenyekiti wa  Mafundi Mizani waliohitimu mafunzo ya utengenezaji wa mizani ya kisasa, Mpasi Hassan ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Henecha Scale alisema,  mafunzo hayo ni muhimu kwao hasa nyakati hizi za mabadiliko ya kiteknolojia.

Alisema kupitia mafunzo hayo wameweza kujengewa weledi wa kutodha ambao utaweza kuleta mabadiliko na ukuaji wa uchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Sahel, Ally Hazam alisema, teknolojia inabadilika hivyo ni wakati sasa wa kuendana na mabadiliko ili tusiachwe nyuma kibiashara.

Alisema wao kama watengenezaji na watoaji Mafunzo ya mizani wameamua kutumia mizani ya kisiasa ambayo itasaidia wafanyabiashara na wateja wao kupata bidhaa halisi kwa kiwango wanachohitaji.

"Wakati sasa umefika wa kutumia mizani sahihi yenye viwango vinavyohitajika ili kukidhi soko la Afrika Mashariki...naomba wanafunzi mnaosoma somo hili mkawe walimu kwa wengine kwakuwa mizani hii inatoa haki kwa anayeuza na anayenunua,"alisema Hazam.

Naye Naibu Kaimu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaalam, Respius Kasmir, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shahada za awali, alisema Chuo kinatakiwa kitoe mafunzo yanayoendana na matakwa ya walengwa hivyo waliamua kuungana na kampuni ya Sahel kwakuwa Ni wadau muhimu wa mizani.

Alisema chuo hicho ndio pekee Afrika Mashariki kinachotoa kozi ya mizani ambapo nchi ya Kenya nayo huwa wanatoa kozi fupi.

No comments:

Post a Comment

Pages