HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 28, 2019

TAARIFA KWA UMMA KIGONGO BUSISI

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) unapenda kuujulisha Umma kuwa huduma ya uvushaji abiria magari na mizigo katika kivuko cha Kigongo na Busisi Mwanza inaendelea katika hali yake ya kawaida baada ya wataalam wa TEMESA wakishirikiana na watumishi kuondoa magugu maji ambayo yaliziba maegesho ya vivuko hivyo pande zote mbili.

Tukio hilo lilitokea Tarehe 24 Desemba 2019 na kudumu kuanzia saa 11 mpaka saa 12:30 jioni ambapo sehemu ya magugu maji hayo iliondolewa na vivuko kupata njia na kuweza kufanya kazi. 

Hata hivyo Wataalamu hao waliweza kufanya kazi ya kuyaondoa kabisa magugu maji hayo kwa kufanya kazi mpaka usiku wa manane na kufanikiwa kuyatoa yote kuhakikisha huduma ya kivuko inaimarika tofauti na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya leo zikielezea kuendelea kuwepo kwa tatizo hilo. 

Aidha TEMESA inawakumbusha abiria wote kuzingatia matangazo ya usalama yanayotolewa na mabaharia watumiapo vivuko. 


                  Imetolewa na Kitengo cha Masoko Habari na                                                    Uhusiano kwa Umma

TEMESA

28/12/2019

No comments:

Post a Comment

Pages