Na Tatu Mohamed
TAASISI ya
kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala inamshikilia
Katibu Mkuu Wa Chama cha Siasa cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi kwa
kosa kujifanya mtumishi wa Taasisi hiyo na kuomba rushwa ya Sh. Milioni
50.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa
Ilala, Christopher Myava alisema Muabhi alijifanya taasisi hiyo na
kuomba rushwa kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bharya Engeneering &
Contracting Company Limited (BECCO) iliyopo Vingunguti, jijini Dar es
Salaam, Manraj Bharya.
Myava
alisema uchunguzi wa Takukuru umebaini kwamba Muabhi dhumuni lake
lilikuwa kuomba rushwa hiyo ili amsaidie Bharya katika tuhuma zake
zilizokuwa zinamkabili Independent Power Tanzania Limited.
"Mtuhumiwa
alikamatwa Disemba 10 majira ya jioni katika ofisi za kampuni ya BECCO
akiwa amepokea fedha za mtego wa rushwa kiasi cha Sh. 100,000,"
alisema.
Aliongeza kuwa uchunguzi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili sheria ichukie mkondo wake.
"Natoa
rai kwa wananchi kujihadhari na matapeli wa aina hii na kujiepusha nao,
na endapo wakibaini wahalifu wowote wa namna hii watoe taarifa Takukuru
ili uchunguzi ufanyike na watuhumiwa waweze kubainika na kuchukuliwa
hatua stahiki," alisema.
No comments:
Post a Comment