HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 30, 2019

TAMASHA LA TUIPENDE BUYANGO LAFANA

 Mgeni rasmi katika tamasha hilo, Anamaria Ngimbwa, akitoa hotuba yake. 
 Timu zilizoshiriki tamasha hilo, Ruhunga FC na Kikono FC
Mkuu wa Shule ya Sekondari Buyango Salapioni Peter.
 
Na Lydia Lugakila, Kagera

 Tamasha la Tuipende Buyango maarufu kama Buyango Day lafana na kutoa shukrani  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuodoa kiporo cha miaka 5 cha jengo la bwalo la wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buyango iliyopo katika Kata ya Buyango wilayani Misenyi mkoani Kagera.

Kauli hiyo imetolewa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Buyango, Salapioni Peter, wakati akiongoza timu ya wananchi na wadau wa maendeleo katika kata hiyo.

Peter amesema licha ya wananchi pamoja na wadau wa maendeleo wameonyesha ushirikiano mkubwa katika kuchangia miradi ya maendeleo na serikali imesaidia kuondoa kiporo cha muda mrefu cha jengo la bwalo la wanafunzi wa shule hiyo kilichodumu kwa miaka mitano.

Amesema kazi kubwa na mchango wa serikali inayoongozwa na Rais Magufuli ni mkubwa  kwani nguvu za wananchi hazitoshi kukamilisha majukumu yote ya kimaendeleo na kutoa pongezi kwa serikali katika kuchangia maendeleo mbali mbali.

Akitaja mchango wa serikali amesema mwaka 2019 serikali ametoa milioni 25 kwa ajili ya vyumba viwili vya madarasa ya shule ya sekondari Buyango ambapo mwezi machi hadi juni mwaka huu chumba kimoja kimekamilika kwa gharama ya shilingi milioni 12 na laki 5 ikiwa ni pamoja na thamani zake.

"Natoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa udhamini wa ukamilishaji wa vyumba hivyo vilivyoshindwa kukamilika kwa muda wa miaka mitano "alisema mkuu huyo wa shule.

Ameongeza kuwa kupitia umoja wa tuipende Buyango na michango ya mbali mbali atahakikisha anahimiza wananchi na wadau wa maendeleo hasa katika kuweka nguvu ya pamoja kujenga maboma ya vyumba vya madarasa ili hata serikali ikisaidia nao wawe katika hatua nzuri.

Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 432 na kutaja changamoto zilizopo shuleni hapo kuwa ni pamoja na kutokamilika kwa nyumba za walimu.

Akitaja lengo la tamasha hilo  maarufu kama Buyango Day Salapioni Peter amesema  lengo la uwepo wa tamasha hilo ni ambalo ufanyika kila ifikapo Desemba 29 ni kusaidia kuwaunganisha pamoja wadau ili kuweza kuweka mipango mikakati ya pamoja ya kuendeleza kata hiyo katika kujiletea maendeleo yenye tija.

Akisoma lisala ya wana umoja wa tuipende Buyango katibu wa asasi ya tuipende Buyango, Gideon Marciale, amesema wazo lao kubwa ni kuanzisha mfuko wa kata ili kujiletea maendeleo.

Marciale amepongeza mchango wa serikali pamoja na wadau huku akieleza mafanikio ya umoja huo kwa mwaka 2016 ambapo waliweza kutengeneza madawati 91, kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya kafunjo, kumlipa Mwalimu wa kujitolea katika shule ya Sekondari Buyango.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika tamasha hilo, Anamaria Ngimbwa amewataka wadau hao kuendelea kujitoa kwa moyo kuliko kusubiri msaada toka serikalini.

Ngimbwa ameongeza kuwa mshikamano wa pamoja unahitajika ili kuinua kata hiyo ki maendeleo.

Naye Diwani wa kata hiyo, Regina Rwamuganga amewahimiza wadau kuongeza juhudi katika kuchangia maendeleo.

Hata hivyo tamasha hilo limeenda sambamba na michezo wa Mpira wa miguu kati ya timu ya Ruhunga FC na Kikono FC ambapo timu ya Ruhunga FC imeibuka kidedea kwa kuicharaza kikono FC kwa 3-0.

No comments:

Post a Comment

Pages