Na Faraja Ezra
KAMISHNA
Mkuu wa Bima Tanzania Dkt. Mussa Juma amezindua rasmi Umoja wa Chama
Cha Mawakala wa Bima Tanzania kwa ajili ya kupanua soko la Bima
nchini.
Aidha Dkt. Juma
alisema ni jukumu la kila Wakala kujitoa na kuendeleza ushirikiano na
kufanya kazi kwa uaminifu ili kuchangia maendeleo ya Taifa.
Pia
amewataka Mawakala wa Bima kuwasilisha Mawasiliano yao katika Mamlaka
ya Bima ndani ya siku saba vinginevyo sheria kali itakuchukuliwa dhidi
yao.
Alisema Chama Cha Mawakala wa Bima kimesajiliwa rasmi na na Msajili mkuu wa Chama na kutambulika rasmi kisheria.
"Agizo
hili ni rasmi na kamawakala hatawasilisha Mawasiliano hayo ndani ya
siku hizo tajwa atachukuliwa hatua stahiki za kisheria," alisema Dkt.
Juma.
Hata hivyo ametoa
wito kwa Mawakala wa Bima kwenda kutoa huduma katika maeneo ambayo
haijafikiwa na huduma ya bima ili kuwanufaisha wadau wa maendeleo
nchini.
Pia Dkt. Juma amesisiza kuongeza idadi ya ajira kwa Mawakala ili kuweza kutoa huduma bora kwa jamii na kuongeza pato la Taifa.
Naye
Mwenyekiti wa Chama Cha Mawakala wa Bima Tanzania Said Daudi,
alisema Chama hicho kinatekeleza majukumu yake ipasavyo kulingana na
sheria iliyowekwa na serikali.
Aidha
Daudi alieleza kuwa wamefanikiwa kutoa huduma bora kwa wadau mbalimbali
katika jamii yangu kimepata ridhaa ya kusajiliwa na Msajili wa Chama.
Licha
ya mafanikio hayo Kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili Chama
ikiwamo, Upungufu wa Fedha, kudharauliwa na baadhi makampuni na
Mawakala.
Ukosefu wa soko la Bima ya maisha katika baadhi ya mikoa nchini ikiwamo Simiyu, Manyara na Tabora.
"Tumekuwa
tukikabiliwa nna changamoto hizi na tumekuwa tukishindwa kutekeleza
huduma zetu kwa wakati muafaka, jambo ambalo limekuwa kero katika
utendaji," alisema Daudi.
Alisema
kutokana ukosefu wa Mawasiliano ya Mawakala katika maeneo ya vijijini
kumeibua Mawakala feki wanaoendelea kutapeli wananchi.
Pia
amewaagiza Mawakala wote nchini kujitoa kufanya kazi kwa uaminifu na
kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa na Mamlaka husika ili
kuboresha utendaji wa kazi na kuinua pato la Taifa.
No comments:
Post a Comment