HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 12, 2019

UMOJA WA CHAMA CHA MAWAKALA WA BIMA TANZANIA UMEZINDULIWA

Na Faraja Ezra

KAMISHNA Mkuu wa Bima Tanzania Dkt. Mussa Juma amezindua rasmi Umoja wa Chama Cha Mawakala wa Bima Tanzania  kwa ajili ya kupanua  soko la Bima nchini.

Aidha Dkt. Juma alisema ni jukumu la kila Wakala kujitoa na kuendeleza ushirikiano na kufanya kazi kwa uaminifu ili kuchangia maendeleo ya Taifa.

Pia amewataka Mawakala wa Bima  kuwasilisha  Mawasiliano yao katika Mamlaka ya Bima ndani ya siku saba vinginevyo sheria kali itakuchukuliwa dhidi yao.

Alisema Chama Cha Mawakala wa Bima  kimesajiliwa rasmi na  na Msajili mkuu wa Chama na kutambulika rasmi kisheria.

"Agizo hili ni rasmi na kamawakala  hatawasilisha Mawasiliano hayo ndani ya siku hizo tajwa atachukuliwa hatua stahiki za kisheria," alisema Dkt. Juma.

Hata hivyo ametoa wito kwa Mawakala  wa Bima kwenda kutoa huduma  katika maeneo ambayo haijafikiwa na huduma ya bima  ili kuwanufaisha wadau wa maendeleo nchini.

Pia Dkt. Juma amesisiza kuongeza idadi ya ajira  kwa Mawakala ili kuweza kutoa huduma bora kwa jamii na kuongeza pato la Taifa.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mawakala  wa Bima  Tanzania  Said Daudi, alisema Chama hicho kinatekeleza majukumu yake ipasavyo kulingana na sheria iliyowekwa na serikali.

Aidha  Daudi alieleza kuwa wamefanikiwa kutoa huduma bora kwa wadau mbalimbali katika jamii yangu kimepata ridhaa ya kusajiliwa na Msajili wa Chama.

Licha ya mafanikio hayo Kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili Chama ikiwamo, Upungufu wa Fedha, kudharauliwa na baadhi makampuni na Mawakala.

Ukosefu wa soko la Bima ya maisha katika baadhi ya mikoa nchini ikiwamo Simiyu, Manyara na Tabora.

"Tumekuwa tukikabiliwa nna changamoto hizi na tumekuwa tukishindwa kutekeleza huduma zetu kwa wakati muafaka, jambo ambalo limekuwa kero katika  utendaji," alisema Daudi.

Alisema  kutokana ukosefu wa Mawasiliano  ya Mawakala katika maeneo ya  vijijini kumeibua Mawakala feki wanaoendelea kutapeli wananchi.

Pia amewaagiza Mawakala wote nchini kujitoa kufanya kazi kwa uaminifu na kuzingatia  taratibu na sheria zilizowekwa na Mamlaka husika ili kuboresha utendaji wa kazi na kuinua pato la Taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages