HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 08, 2019

Wanakikundi cha Mungu yulee wajitokeza kuchangia damu

 Baadhi ya wanakikundi wakichangia damu.


Na Janeth Jovin

KIKUNDI kinachofanya matendo ya huruma kijulikanacho kwa jina la Mungu yule kimewataka wananchi kuongeza juhudi ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa hasa ya mama na watoto.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na wanachama wa kikundi hicho wakati walipojitokeza katika Kanisa Katoliki Magomeni kwa lengo la kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaoteseka mahospitalini kwa kukosa damu.

Akizungumza mara baada ya zoezi hiyo mmoja wa wanakikundi hicho, Yusta Edimund anasema wananchi wenye moyo wa kuchangia damu kwa hiari huokoa maisha ya watu wengi ambao wanahitaji huduma hiyo hivyo wanapaswa kujitokeza kuchangia damu.

“Damu ni uhai, bila ya damu huna uhai huwezi kufanya kazi kama huna damu ya kutosha pia huwezi jua wakati gani utapata tatizo, hivyo tuchangie damu kwa ajili ya wanaohitaji,” anasema.

Aidha anasema ukaguzi unahitajika katika sehemu zote zinazohifadhiwa damu ili kuhakikisha damu ipo katika hali ya usalama na inatumika kama ilivyokusudiwa.

Hata hivyo alisema uchangiaji damu umesaidia kupunguza matatizo mbali mbali ya maradhi na kuongeza kuwa anawashukuru wananchi kwa uelewa na kujitokeza kuchangia damu kwani kila siku mahitaji ya damu yanaongezeka.

No comments:

Post a Comment

Pages