HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 15, 2019

WATU WAWILI WAFARIKI KATIKA SHAMBULIO LA KISU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Revocatus Malimi.

Na Lydia Lugakila Bukoba

Watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika kituo kikuu cha Mabasi cha Bukoba mkoani Kagera baada ya mtu mmoja kuwashambulia kwa kisu kabla ya mtu huyo kuuwawa na wananchi waliokuwa na hasira kali.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, amesema mtu huyo ambaye hajafahamika jina amemshambulia kwa kisu Jofrey Kobadi mwenye umri wa miaka 38 na kumuua papo hapo.

Amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha mtu huyo kuwashambulia watu hao na hivyo kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kufanikisha uchunguzi huo.

‘’Bado tunaendelea kufatilia utambuzi wa huyu mtuhumiwa ambaye kwa sasa ni marehemu alisema’’ kamanda Malimi

Kamanda malimi alisema kuwa baada ya wananchi kuona hali hiyo walimvamia na kuanza kumshambulia kwa kutumia siraha za jadi hadi alivyopoteza nguvu na askari waliokuwa doria mtaani walifika eneo la tukio na kutuliza hali hiyo.

Kamanda huyo amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Salumu Athuman aliyechomwa kisu tumboni na kufanyiwa upasuaji mkubwa, Mico Bukerebe, Jalia Abdu, Jimmy Mashairi na Nasri Abdalla.

Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa Bukoba Dkt Mussa Sweya amekili kupokea maiti mbili na majeruhi watano na kuwa majeruhi wawili wametibiwa na kuruhusiwa kutokana na kuwa na majeraha madogo.

Dkt Sweya amesema Majeruhi watatu wamelazwa hospitalini hapo na mmoja amefanyiwa upasuaji mkubwa baada ya kupata majeraha zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages