December 20, 2019

WAZIRI KABUDI AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Kabudi amemueleza Mhe. Balozi Clavier kuwa, uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa ni wa muda mrefu ambapo hadi sasa Tanzania imekuwa na
mahusiano imara na taifa hilo.

Aidha, pamoja na mambo mengine, mazungumzo yao yalijikita katika kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Ufaransa, kuongeza ushirikino wa maendeleo, kuimarisha uwekezaji, biashara pamoja na kuimarisha masuala
ya ulinzi na usalama. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimsisitiza jambo Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier wakati alipokutana na balozi huyo leo katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Pages