Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Festo Kiswaga, akikata utepe kuzindua duka la Tigo, lililopo Mtaa wa Sokoni wilayani humo. (Na Mpiga Picha Wetu).
NA
MWANDISHI WETU, BARIADI
MKUU wa Wilaya ya
Bariadi mkoani Simiyu, Festo Kiswaga ameyataka makampuni ya simu hapa nchini
kuiga mfano wa Kampuni ya Simu ya Tigo ili kurahisha mawasiliano na huduma
nyingine muhimu.
Kiswaga aliyasema hayo leo wakati akizindua duka jipya la Tigo
wilayani hapo ambapo aliyataka makampuni mengine kusambaa nchini kote ambavyo
tigo imesambaa.
Alisema ufunguzi wa duka
hilo utafungua fursa mbalimbali muhimu za kiuchumi na kuwaomba wananchi wa
wilaya hiyo kulitumia kwa faida.
“Tigo wanapaswa kupongezwa kwani wanafanya
mambo makubwa na mazuri kwa wananchi hivyo ni jukumu la wadau wote wa
mawasiliano kuangalia fursa hiyo kwa jicho la faida,” alisema.
Kiswaga alisema
uwekezaji ambao umefanywa utaboresha huduma na kuhakikisha zinakidhi viwango
vya kimataifa.
“Huduma bora kwa wateja
ni kitovu cha biashara na zaidi huwafanya wateja wajisikie wanathaminika na
kuheshimiwa, Tigo wametekeleza jambo hili kwa vitendo kwa kufanya uwekezaji
katika utoajiwa huduma zao jambo linalowapa utofauti wa kipekee sokoni,”
alisema.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati alisema
hatua ya kufungua duka hilo ni moja ya mkakati wa Tigo wa uboreshaji wa huduma
na kuhakikisha zinawafikia wateja kwa wakati nchi nzima.
Alisema duka hilo
litatoa huduma zote muhimu kuanzia usajili wa namba za simu kwa alama za
vidole, huduma za kifedha ‘Tigo Pesa’ na mauzo ya data na vifaa vya mawasiliano
kama simu janja, router na modem kwaajili ya huduma ya Tigo Home internet.
“Duka hili jipya
litampa mteja wetu wasaa wa kutazama na kujaribu bidhaa mbalimbali kabla ya
kuamua kufanya manunuzi.
Hatua hii imekuja
kufuatia maombi ya muda mrefu kutoka kwa wateja wetu waliokuwa wakihitaji uwepo
wa duka letu kwenye jengo hili maarufu kibiashara hivyo tumekidhi mahitaji
yao,”alisema Madati.
Alisema duka hilo linakuwa
la nne kufunguliwa mkoani humo huku likiwa na huduma mpya ikiwamo simu
zinazotamba kwa sasa aina ya Kitochi 4G Smartpamoja na vifaa vya huduma za
intaneti kwa makampuni maarufu kama ‘Tigo business’.
No comments:
Post a Comment