HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2020

WAJUMBE WAPYA BARAZA LA UONGOZI CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI WAFANYA ZIARA CHUONI HAPO

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi, Prof. Zacharia Mganilwa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa ziara ya wajumbe wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho,  walipotembelea eneo hilo, ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa shughuli za kiutendaji zinavyoendeshwa.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi, Prof. Zacharia Mganilwa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa ziara ya wajumbe wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho,  walipotembelea eneo hilo, ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa shughuli za kiutendaji zinavyoendeshwa. 

Mwenyekiti wake, Mhandisi Prof. Bavo Nyichomba, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Wajumbe wa Baraza la Chuo hicho walipotembelea chuoni hapo.


Na Mwandishi Wetu

BARAZA jipya la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), likiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhandisi Prof. Bavo Nyichomba leo wamefanya ziara ya kwanza katika chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa shunghuli za kiutendaji zinavyoendeshwa chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo, Prof. Nyichomba, amesema lengo la ziara hiyo ni kuwapitisha wajumbe wapya wa Baraza kufahamu jinsi chuo kilivyo, maeneo mbalimbali ya chuo na vitengo vyake na namna ambavyo shughuli za kiutendaji zinafanyika chuoni hapo ili waweze kupata wasaa mzuri wa kutoa ushauri wao .

“Leo tumekuja hapa kuweza kuwapitisha wajumbe wapya ambao waliteuliwa na Mhe Rais John Magufuli, ili wajue nini kilichopo nini kinafanyika ili waweze kutoa ushauri mzuri katika Baraza letu la Uongozi wa chuo hiki.

“Tunategemea kutembelea maeneo mbalimbali ya kufundishia, sehemu ya kujifunzia vitendo vya kazi na majengo mbalimbali ambayo yanatumika kwa mafunzo ya Ndege, Reli na sehemu nyingine za kukagua magari baada ya hapo Baraza litapata wasaa wa kuongea na Chuo hiki.”amesema

Naye  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa, amesema Chuo chao kinajukumu la kuzalisha rasilimali watu ili kuendana na kasi ya Serikali ya tano ambayo imejidhatiti katika kukuza na kuboresha sekta ya uchukuzi na usafirishaji.

“Tunafahamu Serikali ya awamu wa tano ina miradi mikubwa inayotekeleza katika sekta ya uchukuzi na usafirishaji. Jukumu la chuo ni kuzalisha wataalamu stahiki wenye sifa na weledi wa kuweza kuendesha mashirika ya serikali ambayo yamefanyiwa uwekezaji,
“Siku ya leo tuna Baraza la Uongozi la Chuo jipya, ambapo Rais alimteua Mwenyeki na Mhe Waziri akawateua wajumbe, ili waweze kusimamia menejimenti ya Chuo ni vyema wakatembea wakifahamu chuo kwa maana ya kuangalia miundombinu na sughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Chuo.”amesema

No comments:

Post a Comment

Pages