Muonekano wa Barabara ya Sabasaba , Kiseke ,Buswelu iliyojengwa na
wakala wa barabara za Vijijini na Mijini- TARURA Ilemela Jijini Mwanza.
Na, Geofrey Kazaula
Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege ameelezea kuridhishwa kwake
na miradi ya barabara iliyotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na
Mijini Tarura katika Manispaa ya Ilemela
Jijini Mwanza.
Aliyasema hayo wakati
wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Mwanza ambapo
ameeleza kuwa mafanikio yanayopatikana katika Manispaa hiyo hasa katika miradi ya barabara yanatokana
na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wataalam wa TARURA na watumishi wengine wa Manispaa kwa kufanya
kazi pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.
‘‘ Wote tumeshuhudia
barabara hizi zilivyo kwenye kiwango, mafanikio haya yanatokana na Umoja uliopo
kwa watumishi wote wa Manispaa ya Ilemela pamoja na watumishi wa TARURA kwani wanafanya kazi kwa pamoja ili kuwaletea
wananchi wetu maendeleo, kiujumla wanafanya vizuri’’Kandege.
Aidha amesisitiza kuwa
miundombinu ya barabara inapokamilika ilindwe kwa nguvu zote na amewaagiza
viongozi husika huhakikisha barabara hizo zinafanyiwa usafi mara kwa mara na kulinda
miundombinu ya barabara hizo.
Naye Meneja wa TARURA Manispaa
ya Ilemela Mhandisi Clement Kihinga amesema kuwa barabara hizo zilizotekelezwa
chini ya mradi wa Tanzania Strategic Cities Project (TSP) zimekuwa na mafanikio
makubwa ikiwemo kuinua uchumi wa wananchi na kuboresha kiwango cha maisha ya
wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha
wanailinda miundmbinu ya barabara ilizidumu na ziendelee kuboresha maisha yao
na kurahisisha suala la usafiri na usafirishaji katika Manispaa ya Ilemela.
‘‘Serikali inatumia
gharama kubwa sana kujenga barabara hizi hivyo nitoe wito kwa wananchi
kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki kulinda miundombinu hii ya barabara ’’
amesema Mtaalam huyo.
Mmoja wa wananchi wa
Kiseke A Ilemela Issa Shabani alisema awali usafiri ulikuwa changamoto sana Katika
barabar yao kwani miundombinu ilikuwa mibovu sana ila baada ya baraba ya kiseke
Busweru kukamilika maisha yamepanda kiuchumi
“Sasa nafanya biashara
yangu ya matunda hapa Busweru, nayabeba salama na hayaharibiki kwani barabara
ni nzuri na hata kipato changu kimeongezeka hivyo naishukuru sana Serikali kwa kujenga barabara hii”Alisema Shabani
Ziara ya Mhe, Kandege
inaendelea Mkoani Mwanza ambapo miradi mbalibali ya maendeleo zikiwemo barabara
zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA inatarajiwa
kukaguliwa.
No comments:
Post a Comment