Mkurugenzi wa Kitengo cha Vodacom Business, Arjun Dhillon (kushoto), akichangia mada kwenye mdahalo wa teknolojia ya kilimo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Ubunifu uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo mkulima anaweza kupata taarifa mbalimbali za kilimo kupitia mtandao wa Vodacom. Wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geofrey Kirenga na Mshauri wa Sera za Kilimo, Prof. David Nyange. (Na Mpiga Picha Wetu).
Mtaalam na Mshauri wa Teknolojia kwa Wateja wakubwa kutoka Vodacom, Goodluck Moshi, akielezea namna mfumo maalum wa kidijita M-KULIMA utakavyowawezesha wakulima kupata dondoo za kilimo kutoka mtandao wa Vodacom.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi, akizungumza kwenye kongamano la wadau wa kilimo kupitia ubunifu wa kiteknolojia kwa mkulima kuweza kupata taarifa za kilimo, ushauri, bei za mazao, pembejeo na taarifa za hali ya hewa kupitia mfumo maalum wa kidijitali M-KULIMA kutoka mtandao wa Vodacom.
Wadau wa kilimo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali.
Picha ya pamoja mara baada ya kongamano.

Na Irene Mark
SERIKALI imeipongeza Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kubuni huduma rahisi itakayomsaidia mkulima kupata taarifa za hali ya hewa, pembejeo na masoko.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari, Kenneth Bengesi alitoa pongezi hizo Dar es Salaam leo Machi 11,2020 wakati wa Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo (HDIF).
Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, mkurugenzi huyo alisema serikali inathamini bunifu mbalimbali na kuhamasisha nyingine hasa kwenye sekta ya kilimo.
Alisema ubunifu wa Vodacom utasaidia kuinua sekta hiyo ambayo ni uti wa mgongo kwenye uchumi wa taifa kwa kuwa inaajiri asilimia 70 ya vijana ambao nduo nguvu kazi ya nchi.
"Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 27 ya pato la taifa licha ya ukuaji wake wa asilimia tatu kila mwaka... Serikali inaamini ubunifu ukiongezeka kwenye mikakati ya wizara, kilimo kitakuwa bora zaidi na chenye tija," alisema Bengesi.
Alisema serikali imedhamiria kuwekeza zaidi kwenye miundombinu ya ubunifu na teknolojia kwenye kilimo kuanzia shambani hadi sokoni.
Mtaalam Mshauri kwa Wateja Wakubwa wa Vodacom, Goodluck Moshi alisema huduma hiyo ya ubunifu inaitwa M-Mkulima imelenga kuondoa changamoto za ukosefu wa taarifa muhimu za kilimo.
"M-Mkulima inatumika mahali popote hata sehemu chache ambazo hazina mtandao, mkulima anaweza kupata habari sahihi za hali ya hewa, mbegu, mbolea na pembejeo nyingine za kilimo hadi taarifa za soko.
"Hatujabadilisha utaratibu tulichofanya ni kusogeza taarifa muhimu za kilimo kwa wakulima wetu wote... tumewalenga zaidi wakulima wadogo ambao ndio wengi hapa nchini," alisema Moshi.
Akifafanua zaidi alisema ni huduma isiyo na gharama kwa mkulima anayetumia mtandao wa Vodacom.
No comments:
Post a Comment