Na Irene Mark
TAASISI isiyo ya Kiserikali inayofundisha Panya Kutatua Matatizo ya Kibinaadamu (APOPO), imegundua uwezo mkubwa wa panya buku kubaini vimelea vya Kifua Kikuu kwenye sampuli zilizoshindikana hospitali.
Panya buku hao ni wale waliopatiwa mafunzo maalum ya miezi nane hadi 12 kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo mkoani Morogoro.
Hayo yalielezwa kwa wanahabari Dar es Salaam jana kwenye Maonesho ya Wiki ya Ubunifu iliyoandaliwa na Mfuko wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Watu (HDIF) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia mradi huo, Dk. Joseph Soka, alisema walianza kushirikiana na hospitali na vituo vya afya tangu mwaka 2007, wakati huo sampuli zilikuwa zinapelekwa Morogoro kutoka Dar es Salaam.
"Awali sampuli zilikuwa zianasafirishwa kwenda Morogoro kwaajili ya kupimwa na panya kisha kuthibitishwa kwa teknolojia zilizopitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
"...Tulipata changamoto ya ucheleweshaji wa majibu kutoka Morogoro kurudi Dar es Salaam yalikuwa yanachukua kati ya siku nane hadi 10 tukaomba na kupata ufadhili HDIF, walituwezesha ufadhili na tukajenga mahabara hapa jijini kwa lango la kupunguza muda wa kupata majibu kwa mgonjwa hadi siku moja, kuongeza idadi ya sampuli na kuongeza vituo vya afya zaidi.
"Novemba mwaka 2016 tulianza kazi rasmi Dar es Salaam. Tunapata wasani wa sampuli 210 kwa siku kutoka kwenye vituo 53 zikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mloganzila, Hospitali zote za Rufaa za jijini hapa na vituo vya afya na zahanati zote za serikali na binafsi ambazo zina pima kifua kikuu.
"Majibu yetu yamekuwa yakitolewa ndani ya saa 24 baada ya kupata sampuli ya mgonjwa. Ubunifu huu unarahisisha kazi kwa sababu panya buku anauwezo wa kupima sampuli 100 ndani dakika 20 wakati ukitumia darubini itamlazimu Mteknologia wa Mahabara mmoja kufanya kazi hii kwa wiki moja," alisema Dk. Soka.
Kwa mujibu wa Dk. Soka, wanachopata hospitali ni zile sampuli za Kifua Kikuu ambazo zimeonekana kwenye mashine hazina maambukizi ya kifua kikuu hivyo huzipima tena kwa kutumia panya buku hao na sampuli zinazobainika, zina thibitishwa kwa teknolojia ambazo WHO imepitisha zitumike kwenye upimaji wa kifua kikuu.
"Kitaalam tunaita (Concentrated Smear Microscope) na endapo sampuli zitaonesha zina maambukizi ya kifua kikuu, zinarudishwa hospitali husika kwaajili ya mgonjwa kuanza matibabu," alisisitiza Dk. Soka.
Alisema wanafanyakazi kwa karibu na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mpango wa Taifa wa Kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) na Taasisi ya Mapambano ya Kifua Kikuu na Ukimwi Temeke (MUKIKUTE) wanaosaidia kuwatafuta wagonjwa waliodhibitika kuwa na kifua kikuu kwaajili ya kuanza matibabu.
Mkuu wa Mradi wa TB kutoka Apopo, Lena Fiebig alisema kati ya mwaka 2007 walipoanza hadi July 2019 walipima sampuli 591,878 zinazodhaniwa kuwa na Kifua Kikuu, wagonjwa waliobainika kuwa na kifua kikuu ni 15,679 na kufanikiwa kukinga maambukizi mapya kwa watu 121,410 .
"Tunasema tumeokoa maisha ya wagonjwa hawa kwa sababu ni wale ambao hospitali walisema sampuli zao hazina maambukizi ya Kifua Kikuu lakini baada ya kutumia panya buku wetu, tulibaini na kuwarudisha hospitali kwa matibabu zaidi," alisema Fiebig.

No comments:
Post a Comment