Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wanawake wa seMwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Wanawake wa Serikali na Afya (TUGHE), Mkoa wa Pwani, Catherine Katele (kulia), akimkabidhi msaada wa magunia ya mahindi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji, Maria Katemana, kwa ajili ya kuwapatia wananchi waliopata maafa ya mafuriko kutoka na mvua zilizonyesha hivi karibuni. (Picha na Victor Masangu).
Victor Masangu, Rufiji
Baadhi ya wananchi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamekosa
makazi ya kuishi kutokana na nyumba zao pamoja na maduka kuzingirwa na maji ikiwemo wengine kukumbwa na changamoto ya
mazao yao mbali mbali zaidi ya hekta
4000 kusombwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha
maafa hayo ambayo yamepelekea wananchi
kuishi katika mazingira magumu hivyo
kupelekea kuishi katika mazingira magumu.
Hayo yalibainishwa na
wananchi hao wakati wa ziara ambayo imefanywa na Wanawake wa chama cha wafanyakazi wa serikali na afya
(TUGHE) Mkoa wa Pwani yenye lengo la
kutembelea baadhi ya maeneo ambayo
yamekumbwa na maafa ya mafuriko kwa
ajili ya kutoa msaada wa vyakula kwa
walengwa.
Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti akiwemo Shamte
Ally na Said Salumu walisema walidai kwamba mvua ambazo zinaendelea kunyesha kwa kipindi hiki zimewaletea
hasara kubwa ya mazao yao, mifugo, pamoja na makazi kuzingirwa na na maji hivyo
wameimba serikali ya awamu ya tano kuwasaidia msaada wa kupata chakula pamoja na sehemu kwa ajili ya kuishi.
Aidha waliongeza kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa hali
hiyo baadhi ya bidhaa ya vyakula katika maeneo mengine zimepanda bei hivyo
wengine kutokana na kipato chao kuwa cha chini wanashindwa kumudu gharama kwa
ajili ya kununua vyakula hivyo wameomba wadau mbali mbali kwa kushirikiana na
serikali kuliangalia suala hilo kwa jicho
la tatu katika kuwasaidia kuondokana na hali hiyo.
“Kwa kweli ndugu waandishi kwanza tunashukuru sana hawa
wakinamama wa Tughe Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuja mpaka uku katika maeneo ya
Rufiji, kwani kwa sasa tupo katika hali ngumu sana kutokana na mazao mbali
mbali ya chakula ambayo ndio tulikuwa tunayategemea sisi pamoja na watoto wetu
yote wamesombwa na maji, lakini pia tunashukuru kupatiwa msaada huu lakini bado
tunahitaji zaidi ili tuweze kujikimu,” walisema wananchi hao.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria
Katemana alikiri kuwepo kwa maafa hayo
na kubainishwa kwamba hadi sasa zaidi ya
hekta 4000 za mazao ya aina mbali mbali ikiwemo mahindi mpunga,
yamesombwa na maji ambapo pia kuna baadhi ya shule nne za msingi
zimefungwa kwa muda kutokana na kuwepo kwa hali hiyo ya mafuriko
kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha.
“Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu kwa niaba ya
serikali ya Wilaya ya Rufiji kwa msaada huu wa chakula cha mahindi ambao
umetolewa na Wanawake wa Tughe Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwasaidia baaadhi ya
wananachi amabao wamekumbwa na mafuriko hayo ambayo kwa kweli yamesabisha hekta
zaidi ya 4000 za mazao kusombwa na maji
na kuna maeneo mengine ya shule bado maji yapo, hivyo tunaendelea kujitahidi
kwa hali na mali ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao, alisema Maria.
Kufuatia kutokea kwa maafa hayo ya mafuriko Wanawake kutoka chama
cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani wameguswa na tukio hilo na kuamua kwenda kutoa
msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo mahindi kwa wananchi ambao wamekubwa na
maafa ya mafuriko hayo kwa lengo la
kuwasaidia kuweza kupata chakula ikiwemo kupata mbegu kwa ajili ya kupanda tena
kutokana na mazao yao yaliyosombwa na maji.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wanawake wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani
Catherine Katele alisema kwamba waliamua kwenda kutembelea baadhi ya maeneo
ambayo yamekumbwa na mafuriko na kutoa
msaada wa vyakula kama mahindi ambayo yatawasaidia wananchi kuweza kupata
chakula na mengine kuyatumia kwa ajili ya kupanda mazao mengine ambayo yamekwenda na
maji.
“Sisi kama wanawake wa tughe Katika Mkoa wa Pwani kwa kweli
tumegiswa sana na jambo hili la wenzetu wa Rufiji kupata maafa ya mafurikio,
hivyo ktukaona ni vema tufunge safari ya kuja mpaka huku na kweli tumjionea
jinsi ya nyumba mbali mbali ambanzo zimezingirwa na maji na mazao ambayo
yamesombwa na maji kwa hiyo kwa hiki kidogo tulichokitoa cha msaada wa mahindi
kitaweza kuwasaidia kwa namna moja hama nyingine na pia tutazidi kuendelea
kutoa misaada mbali mbali kwa watu wenye mahitaji, “alisema Katele.
Wilaya ya Rufiji iliyopo Mkoa wa Pwani ambayo ina jumla ya
kata zipatazo 13 imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya maafa ya mafuriko hasa
katika kipindi cha mvua zinaponyesha kutokana na baaadhi ya maeneo kuwepo
pembezoni mwa mto Rufiji hivyo kupelekea baadhi ya mazao kusombwa na maji na
nyumba nyingine kuzingirwa na maji na kusababisha wananchi kuishi katika
mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment