HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2020

WANAWAKE TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA (TCDC) WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa tayari kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Jijini Dodoma.
 Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa tayari kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Jijini Dodoma
Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa na Bango la maandamano lenye Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
 Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakibeba bango la maadhimisho mbele ya meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, Jijini Dodoma

=======  ========  ========

Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jumapili 8 Machi, 2020 wameungana na wanawake wengine Duniani kote kuadhimisha siku ya wanawake duniani, Jijini Dodoma.

Wanawake hao wameadhimisha Sikukuu hiyo kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushiriki maandamano yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkonze. Maandamano ambayo yalipokelewa rasmi na Mgeni Rasmi Mhe.Felista Bura (Mb) Kata Mkonze, Jijini Dodoma.

Sherehe hizo zilipambwa kwa Kauli mbiu isemayo “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na baadae” pamoja ujumbe kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika usemao “Wanawake Tuamke na Fursa za Ushirika”

Siku hii maalum huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kukumbuka na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.

Veneranda Mgoba Afisa Ushirika wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika katika mahojiano na waandishi wakati wa maadhimisho hayo ametoa wito kwa wanawake kushiriki fursa zilizopo katika vyama vya Ushirika nchini ili kujiimarisha na hatimaye kuondokana na utegemezi pamoja na umaskini. Akiongeza kuwa ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi bado ni mdogo kulinganisha na wanaume. Hivyo, amewataka wanawake kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vya Ushirika.

“Wanawake wenzangu tujiunge na Vyama vya Ushirika vya kifedha kama vile vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) pamoja na vile visivyo vya kifedha kama vile AMCOS ili kuhakikisha tunapata fursa za kujiendeleza kiuchumi,” alisema Veneranda

Wanawake wa Tume waliendelea na maadhimisho hayo kwa kutoa msaada wa vifaa vya mahitaji mbalimbali kwa wanawake wenzao kwa lengo la kuendeleza upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa wanawake na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages