Mwenyekiti wa Bodi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa Bodi uliofanyika Jijini Dar es Salaam Aprili, 29, 2020.
Wajumbe
wa Bodi wakifuatilia Mkutano wa Waandishi wa Habari na Mwenyekiti wa Bodi ya
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas uliofanyika Jijini Dar es
Salaam Aprili, 29, 2020.
Na Mwandishi Wetu
BODI
ya Utalii Tanzania (TTB) imeainisha mikakati 10 ya muda mrefu inayolenga kuinua
soko la utalii nchini ambalo kwa sasa limeathirika na mlipuko wa ugonjwa wa homa
kali ya mapafu (CORONA) unaosababishwa na kirusi cha (COVID-19) na kuenea katika
nchi mbalimbali duniani.
Hayo
yamesemwa leo Jumatano (Aprili 29, 2020) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa
Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakati wa mkutano na Waandishi wa
vyombo vya habari kuelezea athari za mlipuko ugonjwa wa CORONA na tathimini ya sekta
ya Utalii nchini.
Alisema
kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Utalii Duniani (UNWTO),
inaonesha kuwa mlipuko wa ugonjwa wa CORONA utasababisha kushuka kwa kiwango
cha kati ya asilimia 20-30 ya idadi ya watalii kwa mwaka 2020 pamoja na
kusababisha ukosefu wa mapato kiasi cha Dola za Marekani 300-450 Bilioni
duniani.
Akifafanua
zaidi Jaji Mihayo alisema pia utabiri wa awali uliofanywa na Shirika lisilo la
kiserikali linaloshauri nchi na taasisi za kimataifa la DEFC unaonesha kuwa
mwenendo wa uchumi duniani umebadilika na utaendelea kubadilika ambapo sekta za
utalii na usafiri wa anga ziilizokuwa zimeshamiri, kwa sasa zitakuwa za mwisho
kwenye uchangiaji wa ukuaji wa uchumi duniani.
‘’Sekta
ya Utalii nchini Tanzania inachangia takribani asilimia 17-17.5 ya mapato ya
Serikali (GDP) ambapo kwa mwaka 2018 Tanzania ilitembelewa na watalii wapatao
1,505,702 kutoka watalii 1,327,143 wa mwaka 2017, hivyo janga la virusi vya CORONA limeleta athari
kwenye soko la utalii duniani na hapa nchini pia kwenye sekta zinazowezesha
sekta ya utalii’’ alisema Jaji Mihayo.
Aidha
Jaji Mihayo aliitaja mikakati endelevu iliyowekwa na TTB katika kuendeleza na kukuza
sekta ya utalii nchini ni pamoja na kushirikiana na wadau wa utalii kuandaa
mkakati wa pamoja wa kukabiliana na janga la COVID-19 kwenye sekta ya utalii,
kuandaa mkakati mpya wa mauzo wa kimataifa kupitia ufadhili wa Shirika la
Misaada la Marekani (USAID) na kushirikisha watu mashuhuri na mabalozi wa
utalii Tanzania kwa ajili ya kutangaza utalii.
Aliitaja
mikakati mingine ni pamoja na kuimarisha timu ya mauzo kubuni mbinu za kisasa na
kitaalamu zenye ubunifu wa kuandaa mikakati ya mauzo ya mtandao, kutangaza utalii wa ndani kupitia
programu maalum za mashule na vyuo vya elimu pamoja na kushirikiana na Balozi
za Tanzania nje ya nchi kuweka mikakati bayana ya kuwapata mabalozi wa TTB.
Kwa
mujibu wa Jaji Mihajo alisema mara baada ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa
CORONA, TTB ilianza kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo kuandaa na kurusha
makala fupi ya dakika 1.5 iliyosambaa duniani kuhamasisha watalii kujikinga na
COVID-19 na kuwakumbusha wasifute safari zao za utalii nchini Tanzania.
‘’Makala
hiyo fupi imezunguka kwenye masoko yetu yote makubwa duniani na imevuka
matarajio ya awali ya kiwango cha watu waliyoiona na pia makala hiyo imeoneshwa
kwenye vituo vyetu vya Televisheni na kuwekewa lugha za kiarabu, kifaransa,
kijerumani na kidachi’’ alisema Jaji Mihayo.
Jaji
Mihayo alisema TTB, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya
Uhifadhi Ngorongoro (NCAA) wameingia ubia na kampuni ya Great Migration Camp
kwa pamoja wamebuni kipindi maalum kinachoitwa ‘’Serengeti Live Show’’,
kinachorushwa mubashara na vingine kurekodiwa na kurushwa kwa awamu kwenye
mitandao ya TTB na washirika wake nchini na nje ya nchi kuonesha utalii wa
Tanzania.
Aliongeza
kuwa madhumuni ya vipindi hivyo ni kukonga mioyo ya watalii ambao wameahirisha
safari zao za kuja Tanzania kwa kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa CORONA,
ambapo kupitia vipindi hivyo Tanzania itahakikisha kuwa Jina maalum la
kutangaza utalii wa Tanzania la Tanzania
Unforgettable linaendelea kutumia ili kuhamasisha sekta ya utalii nchini.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devotha Mdhachi alisema mwezi Mei
mwaka huu Ofisi yake inatarajia kufanya kikao na wadau wa sekta ya utalii
nchini ili kujadili mikakati ya pamoja inayolenga kuimarisha soko la utalii
nchini katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiriwa na mlipuko wa ugonjwa wa
CORONA.
No comments:
Post a Comment