April 29, 2020

KALIUA YAFIKISHA ASILIMIA 64 ZA MAKUSANYO YA NDANI

Na Tiganya Vincent
 
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua hadi sasa imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.4 ambayo ni sawa na asilimia 64 ya lengo la  shilingi bilioni 3.8.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Haruna Kasele wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.

Alisema wamefanikiwa kufikisha asilimia hizo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Madiwani na Watendaji wa Halmashauri hiyo.

Aliwataka Watendaji kuendelea kusimamia vema ukusanyaji wa mapato ya ndani ili yaweze kusaidia katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya shule, afya na maji.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisisitiza matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji mapato.

Alisema mfumo huo unasaidia kuzuia wizi na upotevu wa mapato ya ndani yanayotokana na vyanzo mbalimbali.

Aidha Busalama aliitaka Halmashauri hiyo kujenga uzio katika Minada iliyopo ili kudhibiti watu wanaokwepa kulipa mapato kwa sababu ya kukosa uzio.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua alisema katika ukaguzi uliopita wa ofisi ya CAG wamepata Hati safi.
Aliwataka watendaji kuendel;ea kutendaji katika kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia shughuli mbalimbali ikiwemo za malipo.

No comments:

Post a Comment

Pages