Na Tiganya Vincent
HALMASHAURI ya
Wilaya ya Kaliua hadi sasa imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.4 ambayo ni
sawa na asilimia 64 ya lengo la shilingi
bilioni 3.8.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Haruna Kasele wakati wa kikao cha Baraza
la Madiwani.
Alisema wamefanikiwa
kufikisha asilimia hizo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Madiwani na
Watendaji wa Halmashauri hiyo.
Aliwataka Watendaji
kuendelea kusimamia vema ukusanyaji wa mapato ya ndani ili yaweze kusaidia
katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya shule, afya na
maji.
Kwa upande wa Mkuu
wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisisitiza matumizi ya teknolojia katika
ukusanyaji mapato.
Alisema mfumo huo
unasaidia kuzuia wizi na upotevu wa mapato ya ndani yanayotokana na vyanzo
mbalimbali.
Aidha Busalama aliitaka
Halmashauri hiyo kujenga uzio katika Minada iliyopo ili kudhibiti watu
wanaokwepa kulipa mapato kwa sababu ya kukosa uzio.
Katika hatua
nyingine Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua alisema katika ukaguzi
uliopita wa ofisi ya CAG wamepata Hati safi.
Aliwataka watendaji
kuendel;ea kutendaji katika kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia
shughuli mbalimbali ikiwemo za malipo.
No comments:
Post a Comment