Katibu wa Mbunge wa Singida Magharibi, Abubakari Muna (katikati), akikagua ujenzi wa nyumba ya mama na mtoto inayojengwa Kata ya Muhintiri wilayani Ikungi.
Hapa wakipeana maelekezo ya ujenzi huo.
Ujenzi wa choo cha Zahanati ya Kata ya Muhintiri ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu ameendelea kuunga mkono agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kuwataka wananchi kote nchini kuendelea kuchapa kazi katika kipindi hiki ambacho tunakabiliwa na ugonjwa wa corona.
Kingu licha ya kuwa Bungeni amekuwa akiendelea kutekeleza miradi yake ya maendeleo jimboni kwake kwa usimamizi wa Katibu wake Abubakari Muna jambo ambalo limewatia moyo wananchi na kujitojeza kushiriki huku wakichukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya corona.
Akizungumzia na waandishi wa habari juzi, Kingu alisema kazi za maendeleo zinaendelea kama kawaida kama Rais John Magufuli alivyoelekeza.
"Nipo bungeni lakini kazi za maendeleo jimboni zinaendelea na zinasimamiwa na Katibu wangu Muna na wananchi wanajitokeza kwa wingi kushiriki" alisema Kingu.
Alisema miradi inayoendelea kujengwa ni ujenzi wa nyumba ya mama na mtoto na choo cha Zahanati ya Kata ya Muhintiri.
Kingu alisema mradi mwingine ni ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mpetu na Kinyampembee ambao ujenzi wake umefikia ngazi ya linta.
Rais Dkt. Johnn Magufuli alipokuwa akihutubia taifa kuhusu ugonjwa wa corona aliwataka wananchi kuendelea kufanya kazi huku wakichukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.
Alisena hakuna mradi utakaosimama kwa sababu ya kuhofia ugonjwa huo na kuwataka wananchi kila mmoja kufanya kazi ili kuinua uchumi wa nchi yetu.
No comments:
Post a Comment