Waziri wa
Kilimo, Japhet Hasunga (kulia) na Waziri wa Viwanda na Bishara, Innocent
Bashungwa, wakizungumza na waandishi wa habari wakati wakitoa taarifa
kwa umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na
mwenendo wa bei yake katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa
2019/2020. Jijini Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020. (Picha na
Eliud Rwechungura, Wizara ya Viwanda na Biashara).
Waziri wa
Kilimo, Japhet Hasunga (katikati) akitangaza kikomo cha kiwango cha juu cha
bei ya sukari kwa reja reja kwa kila mkoa Wakati wakitoa taarifa kwa umma
wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake
katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020. Kushoto ni Waziri wa
Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa, Naibu waziri Kilimo, Omary Mgumba (kulia).
Waziri wa
Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa (kushoto ), akisisitiza wafanyabiashara
kote nchi kuzingatia kikombo cha bei ya sukari iliyotolewa na Serikali kwa
wafanyabiashara wa reja reja kila mkoa Wakati wakitoa taarifa kwa umma wa
Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake
katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020. Katikati ni Waziri wa
Kilimo, Japhet Hasunga, kulia ni Naibu Waziri Kilimo, Omary Mgumba. jijini
Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020.
Na Eliud Rwechungura – WVB
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na Waziri wa
Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa wamekutana na waandishi wa habari ili kuzungumza na umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali
ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameanza kwa
kueleza mahitaji na matumizi ya sukari nnchi ‘‘Mahitaji
ya sukari ya matumizi ya kawaida Nchini yanakadiriwa kufikia tani 470,000 kwa
Mwaka. Kiasi hiki ni kwa wastani wa mahitaji ya kiasi cha tani 38,000 kwa kila
Mwezi pamoja na kiasi cha tani 14,000 kwa ajili ya dharura.
Uwezo wa viwanda vyetu vya ndani kwa
msimu wa 2019/20 kwa mujibu wa makadirio ya mwanzoni mwa msimu yaani Julai,
2019 ni kuzalisha takribani tani 378,000 za sukari. Kiasi hiki ni sawa na
asilimia 82.9 ya mahitaji halisi ya tani 456,000 ambayo hayajumuishi kiasi cha
dharura cha tani 14,000.
Uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya
ndani unaacha pengo la kiasi cha tani 78,000 ili kuweza kutosheleza mahitaji
halisi ya tani 456,000 bila kiasi cha dharura cha tani 14,000.
Hata hivyo, uwezo huu wa uzalishaji wa
viwanda vya ndani ulitarajiwa kufikiwa pale tu panapokuwa na hali nzuri ya hewa
na ufanisi mzuri wa viwanda’’
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameendelea kwa changamoto ambazo zimekumba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/2020
‘‘Kutokana na ukweli kwamba msimu wa
uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/20 umekumbwa na changamoto kadha wa kadha
zikiwemo
i.
Mvua
nyingi kupita kiasi ambayo imepelekea uvunaji wa miwa kuwa mgumu,
ii.
Mlipuko
wa magonjwa ya miwa kama vile viding’ata wa njano n.k,
iii.
Uharibifu
wa mitambo ya baadhi ya viwanda na kuchelewa kupatiwa vipuri.
Sababu hizo zote kwa pamoja zimechangia
kwa kiasi kikubwa Viwanda vyetu vya ndani kushindwa kufikia malengo ya
kuzalisha tani 378,000 za sukari kwa msimu wa 2019/20.’’
Waziri wa Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa,
ametoa hali ya uzalishaji wa viwanda vya sukari nchini:
Na.
|
Jina la Kiwanda
|
Malengo ya Uzalishaji (tani)
|
Kiasi kilichozalishwa (tani)
|
Uzalishaji (%)
|
1
|
Kilombero Sugar Co. Ltd
|
120,183
|
103,122
|
85.8
|
2
|
TPC Ltd
|
90,815
|
88,968
|
98.0
|
3
|
Kagera Sugar Ltd
|
95,000
|
79,403
|
83.6
|
4
|
Mtibwa Sugar Estates Ltd
|
33,513
|
20,705
|
61.8
|
5
|
Manyara Sugar Co. Ltd
|
5,785
|
6,750
|
116.7
|
JUMLA
|
345,296
|
298,949
|
86.6
|
‘‘Kutokana na hali halisi ya
uzalishaji wa ndani wa sukari kuwa pungufu ya malengo ya uzalishaji, Serikali
ilifanya makadirio ya kiasi cha sukari ya kuziba pengo la uzalishaji (gap
sugar) na kutoa vibali kwa wazalishaji ili kuweza kuagiza na kuingiza sukari
hiyo Nchini kwa wakati kwa ajili ya kukidhi mahitaji. Hadi hivi sasa tunazungumza
na nyinyi, sukari iliyoagizwa kuja kuziba pengo la uzalishaji takribani tani
10,710 imeshaingia nchini na inaendelea
kusambazwa katika Mikoa yote.
Mnamo tarehe 24, 28 na
30 Aprili, 2020 tunategemea kupokea jumla ya tani 13,500 za sukari ya kuziba
pengo na tutaendelea kupokea kiasi kingine cha sukari Mwanzoni mwa Mwezi Mei,
2020. Kiasi chote cha sukari kilichopo Nchini na tunachoendelea kupokea
kinatosheleza kabisa mahitaji ya sukari nchini. Kwa taarifa hii, tuwaombe Wananchi
wote kuwa watulivu kwa sababu Nchi yetu inayo sukari ya kutosha.’’
Waziri wa Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa
amesema serikali haitakubali kuona wafanyabiashara kupandisha bei kiholela
‘‘Tunapenda kuwatangazia Wafanyabiashara
wote Nchini wenye tabia hizi za kupandisha bei kiholela waache mara moja kwani
Serikali haipo tayari kuona Wananchi wake wanaumia kwa manufaa ya watu
wachache.
Serikali itachukua hatua kali kwa
Mfanyabiashara yeyote ambaye atabainika kujinufaisha kwa kuuza sukari bei ya
juu kulikoni bei ya kawaida ya soko.’’
Aitha, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kabla ya
kutangaza bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini amesema;
Kwa
mujibu wa Sheria ya Sukari Na. 26 ya Mwaka
2001(Cap. 251) chini ya kifungu cha 11A inampa Mamlaka Waziri mwenye dhamana ya
Kilimo kutangaza bei ya ukomo wa juu ya sukari.
Kutokana
na changamoto ya wafanyabiashara kupandisha kiholela bei ya sukari nchini, Serikali
tumeamua kuutangazia Umma wa Watanzania bei Kikomo ya sukari katika Mikoa yote
Nchini Tanzania. Bei hizi kikomo zinalenga kukabaliana na changamoto ya kupanda
kiholela kwa Bei ya Sukari Nchini ambayo kwa sasa imefikia wastani wa Shilingi
4,000/= hadi 4,500/= kwa kilo. Bei hii kikomo ya sukari imepangwa kwa
kuzingatia gharama zote za uagizaji wa sukari ya kuziba pengo zinazotumiwa na
wazalishaji kuagiza sukari kutoka nje ya Nchi.
Hivyo,
kwa niaba ya Serikali tunapenda kuutangazia umma wa Watanzania kuwa bei ya sukari
ya reja reja Katika Mikoa yote nchini itakuwa kama ifuatavyo;
KIWANGO CHA JUU CHA
BEI YA SUKARI KWA REJA REJA KWA KILA MKOA
NA.
|
MKOA
|
BEI
YA KILO (Tsh)
|
|
IRINGA
|
2,900
|
|
MBEYA
|
3,000
|
|
RUKWA
|
3,200
|
|
KATAVI
|
3,200
|
|
RUVUMA
|
3,200
|
|
NJOMBE
|
2,900
|
|
LINDI
|
2,800
|
|
MTWARA
|
2,800
|
|
ARUSHA
|
2,700
|
|
KILIMANJARO
|
2,700
|
|
MANYARA
|
2,700
|
|
TANGA
|
2,700
|
|
DAR ES SALAAM
|
2,600
|
|
PWANI
|
2,700
|
|
MOROGORO
|
2,700
|
|
KAGERA
|
3,000
|
|
MWANZA
|
2,900
|
|
SIMIYU
|
2,900
|
|
SHINYANGA
|
2,900
|
|
GEITA
|
2,900
|
|
MARA
|
3,000
|
|
KIGOMA
|
3,200
|
|
SINGIDA
|
2,900
|
|
TABORA
|
2,900
|
|
DODOMA
|
2,900
|
|
SONGWE
|
3,000
|
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amemaliza kwa
kusisitiza kuwa;
‘‘Bei hizi za ukomo za sukari
zimezingatia umbali wa kila eneo katika Mikoa yote nchini. Niwaombe
Wafanyabiashara wote nchini kuzingatia maelekezo haya ya Serikali. Yeyote
atakayekiuka maelekezo haya atakuwa ametenda kosa na hivyo atafikishwa katika
vyombo vya sheria ili apate adhabu ambayo itahusisha ama kunyang’anywa leseni
ya biashara, kulipa faini au adhabu zote kwa pamoja. Tutachukua hatua kali za
kisheria kwa mfanyabiashara yeyote ambaye atakiuka masharti haya.’’
No comments:
Post a Comment