KAMPUNI
ya General Petroleum ya jijini Dar es Salaam imetoa vyakula vya aina
mbalimbali vyenye thamani ya Sh.Milioni 50 kwa kaya zaidi 1,500 za
kipato cha chini ili ziweze kukabiliana na ugumu wa maisha katika
kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 na Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani.
Msaada huo umetolewa na Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Zafar Khan wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Alisema
GP ni kampuni ambayo inapenda kusaidia jamii hivyo imeamua kuungana na
Serikali katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona kwa
kuwapatia wananchi wanyonge chakula na mafuta.
Khan
alisema kwa sasa wemetoa msaada kwa kaya 1,500 za jijini Dar es. Salaam
na Bagamoyo hivyo wanaamini wataweza kusaidi kiasi kuondoa ugumu wa
maisha kwa familia.
"Sisi
kama wadau wa maendeleo ndani ya wilaya ya Temeke na Tanzania na
Tanzania kwa ujumla tumeamua kutoa msaada huu wa vyakula na mafuta kwa
kaya 1,500 kipindi hiki cha mapambano ya ugonjwa wa COVID-19 lakini pia
vitawasaidia kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani," alisema.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo Katibu Tarafa ya Mbagala wilayani Temeke
Betha Minga wakati akipokea vitu hivyo alisema wanawashukuru Kamapuni
ya GP kwa kuwakumba wanyonge katika kipindi hiki.
Minga alisema GP ni wadau wakubwa wa maendeleo wilayani hapo na kuwataka waendelee na moyo huo huo.
Aliema
awali kabla ya kutoa msaada huo ambao unajumla ya ya thamani ya
shilingi zaidi ya Milioni 50 za kitanzania walishatoa vitakasa mikono,
na Barakoa kwa ajili wananchi wa kata 23 za Manispaa hiyo ya Temeke.
"Binafsi
kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Temeke tunawashukuru watu hawa kwani
katika Wilaya yetu wamekuwa na msaada mkubwa Sana Mara zote wamekuwa ni
watu wakujitoa Sana hivyo tunawashukuru Sana na msaada huu unakwenda kwa
watu waliokusudiwa ."alisema Minga.
Alisema
vifaa hivyo vinakwenda katika kata zote zilizopo katika Wilaya ya
Temeke na kila kata watapata vifurushi 20 na tayari tulishaainisha
wanaostahiki kupata hususani katika kipindi hiki ambacho ndugu zetu
waislamu wanaaza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani..
No comments:
Post a Comment