HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 06, 2020

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WATEMBELEA MPAKA WA KENYA NA TANZANIA ENEO LA HOROHORO KUONA HATUA ZINAZOCHUKULIWA

 Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Abdulla Makame akizungumza mara baada ya wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro –Lungalunga kuangalia umeathirika vipi kutokana na janga la Virusi vya Corona na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kuweza kukabiliana nao huku wakiridhishwa na hatua zinazochukuliwa kulia ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure.
  Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Abdulla Makame akisisitiza jambo wakati walipotembelea mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro ikiwemo upande wa pili wa nchi ya Kenya
 Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akifuatilia jambo wakati wa ziara hiyo
 Sehemu ya watumishi wa TRA mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali
 Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Abdulla Makame kushoto akisalimiana na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati walipoingia kwenye Kituo cha Forodha Horohoro

 WABUNGE wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla
Makame na Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa
 WABUNGE wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla Makame na Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa  katikati wakiangalia bidhaa mbalimbali mpakani hapo
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa katikati akinawa na santize kabla ya kuingia kwenye ofisi mbalimbali zilizopo mpakani hapo
 Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akiwa na Mbunge  wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdulla Makame wakitoka nje mara baada ya kufanya ziara yao
 Wakipata picha ya pamoja mara baada ya kutembelea eneo hilo
 Wakiwa kwenye picha ya pamoja na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki


WABUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro –Lungalunga kuangalia umeathirika vipi kutokana na janga la Virusi vya Corona na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kuweza kukabiliana nao huku wakiridhishwa na hatua zinazochukuliwa.

Mpaka wa Horohoro upo wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na Kenya ambao umekuwa ukitumiwa na wananchi wa nchi hizo mbili kuweza kuvuka upande mmoja hadi mwengine lakini hivi sasa inaelezwa huwezi kuvuka bila kuwekwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha siku 14.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo  hivi karibuni Mwenyekiti wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Abdulla Makame ambayo pia walikuwa wameambatana na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure huku akizipongeza mamlaka zilizopo mpakani hapo kutokana na hatua inazochukua kukabiliana na janga hilo lakini kwa kuzingatia taratibu zilizotolewa na Serikali.

Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza watumishi wanaofanya kazi kwenye sekta ya afya nchini kutokana na kuwa mstari wa mbele kutoa huduma ikiwemo kuweka maisha yao rehani kuhakikihs wanatuokoa na janga hilo hatari ambalo limekuwa tishio kubwa duniani.

Aidha alisema mpaka sasa nchi haijafunga mipaka yake na watu wanaendeela kuvuka lakini kwa tahadhari ya afya wanaovuka wataendelea kuwekwa chini ya uangalizi kwa siku 14 ili waweze kujiridhika kama ana maambukizi au la .

“Mpaka sasa hapa kwetu nchi haijafunga mipaka yake sababu serikali inataka bidhaa muhimu ikiwemo vifaa tiba kwa kipindi hiki vinahitajika vitaendelea kuvuka lakini watu wanaovuka watakwenda karatini”Alisema Dkt Abdulla.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba sio kwamba watu wanazuiwa ili waonewe wanachoifanya ni kupambana na janga la kitaifa ambalo limefanya mataifa makubwa watu wanalia, wanakufa hali ni hatari na lazima hatua hizo zichukuliwe.

“Lakini pia tumeambiwa hapa kwamba abiria wakivuka wanakaa karantine siku 14 katika uangalizi kabla ya kuvuka tumeonyeshwaa maeneo na mengine tumeambiwea yapo Tanga mjini kabla ya kuendelea na safari zao hilo zoezi lilikuwa ni kuangalia abiria”Alisema

“Madereva walikuwa na utaratibu tofauti kwa sababu wanapeleka mizigo na walisema hawataki mizigo isivuke kutokana na baadhi yake ni vifaa ikiwemo tiba na vyakula ambavyo vinahitajika kila siku na kuweka maisha yakawe sawasawa “Alisema

Mwenyekiti huyo alisema kwamba lakini waraka namba 2 umetoka na kwa sasa madereva nao watakuwa wakikaa karantine huo waraka utaanza kutekeleza kutokana na hilo wameona maelekezo yanazidi kuwa makali lakini pamoja na ukali wanasema mipaka bado ipo wazi na bidhaa muhimu zitaendelea kuvuka.

Hata hivyo alisema watatumia utaratibu mwengine kwamba ama gari zishushe mizigo mipakani ipandishwe magari mengine au gari ije ibadilishe madereva mipakani na kuwekwa dawa na madereva kubaki kwenye nchi zao.

“Kimsingi maelekezo ya serikali yanaendelea kufuatwa na mpaka sasa kwenye mpaka huo hajapatikana mgonjwa yoyote wa Corona lakini tumeambiwa wapo karatine watu 47 na watu wanne walishukiwa kuonyesha dalili walipimwa wakawa hawana na waliruhusiwa”Alisema

Awali akizungumza kwa upande wake Mbunge mwengine wa Bunge hilo Mhandisi Mohamed Habibu Mnyaa alisema wamefika eneo hilo kwa lengo la kuona uelewa upo kiasi gani na taratibu zilizotangazwa na serikali za kujilinda na virusi vya Corona umeeleweka kiasi gani na watu wanayafuata kwa kiasi gani.

Alisema wao kama wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wamelazimika wote kufanya kazi ndani ya nchi zao kushirikiana na serikali na wananchi kuhusu kupiga vita maradhi ya virusi vya Corona kwa hiyoi kwa upande wa Tanzania wamegawana vikundi vya watu wawili wawili maeneo mengine mmoja kutembelea mipaka mbalimbali iliyopo nchini lengo kusaidia uelewa wa wananchi kupiga vita maradhi hayo.

 Naye kwa upande wake Afisa Afya Mfawidhi Huruma Kimaro alisema katika mpaka huo hakuna mtu yoyote anayepita na wanaofika hapo wanapelekwa karatini na mpaka sasa watu 47 wapo karatine huku akieleza kwamba walipata washukiwa wanne walipopelekwa maabara walikuwa hawajaambukizwa waliwaruhusu na kuwapa maelekezo ikiwemo kutoa ushauri kwao kwa kuendelea kuwa mabalozi wazuri.

No comments:

Post a Comment

Pages