Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati wakipewa maelezeo ya uzalishaji kiwandani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati, Dustan
Kitandula, akipewa maelezo na Mkurugenzi mwenza wa AFRICAB, Yusuf Ezzi, kuhusu
uzalishaji unaofanywa na kiwanda hicho.
Mtendaji Msaidizi wa AFRICAB, Gina Kunjal, akifafanua jambo kwa kuhusiana na uzalishaji wa kiwanda
hicho.
Mkurugenzi mwenza wa AFRICAB, Yusuf Ezzi, akitoa maelezo kwa wajumbe
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati wakipewa maelezeo ya uzalishaji
unaofanywa na kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa AFRICAB, Mansoor Moiz na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Subira Mgalu wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa AFRICAB, Mansoor Moiz na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Subira Mgalu wakati wa ziara hiyo.
Na Mwadishi Wetu
KATIKA kuendelea
kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu
ya tano ya uharakishaji katika ujenzi wa
miundombinu ya umeme nchini, Kampuni ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya
umeme ya Kilimanjaro Cables ‘AFRICAB’ inatarajia kufunga mitambo mipya 10 itakayowezesha uzalishaji wa nyaya za
umeme mara mbili kutoka uzalishaji wa sasa.
Hatua hiyo pamoja na mambo mengine inatajwa na Kampuni hiyo
kuwa itasaidia usambazaji wa umeme huo inayofanywa kupitia Wakala wa Usambazaji
wa Umeme Vijijini (REA) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwenda kwa
kasi kama ilivyoagizwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati iliyotembelea
kiwandani hapo hivi karibuni kujionea uzalishaji unaofanyika.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho Mansoor Moiz, kufungwa kwa mitambo hiyo mipya
na ya kisasa, kutakiwezesha kiwanda hicho kufikia uzalishaji nyaya kutoka wastani wa Kms 37,500
za sasa hadi kms 75000 ifikapo Julai Mwaka huu na hivyo kuongeza ufanisi katika
miradi hiyo na mengineyo inayotumia bidhaa za kampuni hiyo.
“Tunafanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali yetu
ambayo kwa sasa tunashuhudia inafanya kazi kubwa ya kusambaza umeme maeneo
mbalimbali ya nchi,tunafanya kazi ya
uzalishaji usiku na mchana lengo ni kuhakikisha tunawasaidia wakandarasi wote
waliopo katika miradi hiyo kufanya kazi zao kwa uhakika kulingana na muda”
alisema Moiz.
Alisema kiwanda hicho
kilichoanzishwa Mwaka 2001 kama mtengenezaji wa nyaya za majumbani , kwa sasa
kinazalisha wastani wa Mita 6900 za nyaya za kuchoronga(Drawing), nyaya za
kuvishwa(Insulting) KMS 18,000 na kusukwa(Stranding) KMS 37,500 pekee na
kuongeza kuwa kufungwa kwa mitambo hiyo mipya kutakiwezesha kiwanda hicho
kuzalisha mara mbili ya idadi hiyo ya sasa.
Akizungumza wakati wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati
ilipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dustan
Kitandula, aliutaka uongozi wa kiwanda hicho cha AFRICAB kuongeza uzalishaji
ili kuwawezesha wakandarasi wa miradi ya umeme inayotekelezwa na Serikali
kuendana na kasi.
Mbali ya kupongeza juhudi ya kiwanda hicho kwa uzalishaji
inaoufanya, alisema kuna haja ya AFRICAB kuona namna ambavyo itazidi kuongeza
kasi ya uzalishaji ili kuzidi kuharakisha kasi ya miradi hiyo kwa ajili ya
maendeleo ya nchi.
“Tutaendelea kufanya kazi katika mwelekeo wa kuanzisha
vitengo vya viwanda ili kukidhi mahitaji ya soko la umeme Tanzania kwa kuwa
tumechagua kuwa kituo kimoja cha suluhisho la utoaji wa mahitaji yote ya umeme
nchini na Afrika Mashariki” alisema Moiz
Mbali na uzalishaji wa nyaya, kiwanda cha AFRICAB pia
kinazalisha vifaa mbalimbali vya umeme wa majumbani, Isolators pamoja na
Transfoma ambazo kwa wastani kiwanda hicho kinazalisha Transfoma 6500 kwa
Mwaka.
Aidha Moiz aliwataka wazalishaji wengine kuendelea
kushirikiana kwa pamoja kuzalisha bidhaa
zenye ubora ili kulinda soko la ndani na hivyo kulitangaza taifa nje ya mipaka
yake kwa kuwa na bidhaa zenye kumlinda mlaji.
Alisema mahitaji la ya bidhaa mbalimbali za umeme katika
soko bado ni kubwa hivyo kuna kila sababu ya wazaalishaji wote kufanya kazi kwa
umoja ili kuongea tija badala ya kushindana ambapo madhara yake makuu ni
kuzalisha bidhaa zisizo na ubora kwa kigezo cha kukimbilia soko.
No comments:
Post a Comment