Mwanasheria na Wakili maarufu nchini Albert Msando akikabidhi vitakasa
mikono 100 na barakoa 100 kwa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa
Arusha (APC) kwenye Makao Makuu ya APC jijini Arusha leo.
Wakili Albert Msando, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC ) mara baada ya kukabidhi barakoa 100 na vitakasa mikono 100 kwa ajili ya
wanahabari kutekeleza majukumu yao. (Picha na Ahmed Mahmoud Arusha).
Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Imeelezwa
kuwa Waandishi wa habari nchini wapo kwenye kipindi kigumu cha
kutekeleza majukumu yao wakati huu wa mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19
kiuchumi na wadau wametakiwa kujitokeza kusaidia kada hiyo ili iweze
kutoa taarifa sahihi na kweli.
Kwa
mujibu wa mdau wa maendeleo jijini Arusha Mwanasheria Maarufu, Albert
Msando na mmiliki wa The Don ambaye ametoa barakoa na vitakasa mikono
kwa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC) ikiwa ni kusaidia
mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.
Msando
akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo amesema kuwa kada ya
uandishi wa habari ni muhimu sana kutoa taarifa za ugonjwa wa Covid-19
lakini wao wamekuwa wakishindwa kutoa taarifa kutokana na changamoto zao
kipindi hiki cha janga la corona
Aidha
alisema kuwa imekuwa shida sana kupata taarifa sahihi za ugonjwa huu
huku hali ikiwa inazidi kuwa mbaya na kipindi hichi jamii inahitaji
taarifa zaidi ili kuiondoa kwenye taharuki ni muhimu kwao wanahabari
kuwezeshwa hata nauli ya kutoka eneo moja kwenda jingine itaisaidia
jamii kupata taarifa sahihi sio bora taarifa.
Alisema
kuwa ni muhimu kwa waandishi kupata taarifa sahihi kutoka vyanzo husika
na kuzitoa utaona ni Jambo dogo Ila kila moja amekuwa na taharuki
kutaka kujua taarifa kupitia kwenu nanyi ni watu muhimu Sana ikitoka
wataalamu wa Afya ni nyinyi.
"Wadau
wajitokeze kusaidia kwani waandishi wa habari wapo katika wakati mgumu sana kiuchumi katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Covid 19 na jamii
inahitaji taarifa za hali ya ugonjwa huo huku waandishi wakiwa taabani
kiuchumi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku"alisisitiza
Aliwataka
waandishi wa habari kusema ukweli kuhusu idadi ya watu wanaokufa
waliopata ugonjwa wa Covid 19 kwani jamii inapata taarifa sahihi kutoka
kwao hivyo Amewataka kutumia uwezo wao wote na kufanya kazi hiyo kwa
weledi.
Aliwakumbusha wadau
wa maendeleo kuendelea kusaidia waandishi wa habari ili waweze kuwapatia
wananchi taarifa za kina na sahihi kuhusiana na janga hili ili kuondoa
taaruki miongoni mwa jamii.
Naye
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, Claud Gwandu,
alimpongeza Mdau huyo kwa msaada wake huo na kuwataka wadau wengine
kujitokeza kusaidia kada hiyo
Alimshukuru mdau huyo kuikumbuka kada hiyo na kuona umuhimu wao wa kuwapatia
vitendea kazi hivyo kipindi hichi cha janga la Corona ambavyo
vitawafanya kufanya kazi zao wakati huu wa janga la ugonjwa wa Covid-19.
No comments:
Post a Comment