Wizara ya Kilimo imekubaliana na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine kuanza
kuzalisha mbegu boraza mazao ya kilimo ili kujitosheleza na mahitaji ya
wakulima nchini.
Makubaliano
hayo yamebainishwa leo (24.04.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Gerald Kusaya alipokutana kwa mazungumzo na Menejimenti ya Chuo hicho
mjini Morogoro na kueleza kuwa nchi bado haijajitosheleza na mbegu bora.
“Tunahitaji
ushirikiano wa kuzalisha mbegu bora za mazao ya kilimo kwa wingi ndani
ya nchi ili kukidhi mahitaji ya wakulima ” alisisitiza Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo inapenda chuo Kikuu cha Sokoine kianzishe vitalu vya
uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga mboga na matunda ili kupunguza
utegemezi toka nje ya nchi.
“Ifike
hatua nchi yetu kuwa na uhakika wa mbegu bora na hai.Hii itaongeza
ajira kwa vijana na wakulima kupata manufaa” alisema Katibu Mkuu Kusaya
Kusaya alitaja maeneo mengine ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sokoine
kuwa ni kuanzisha maabara bora ya kilimo ili kusaidia mapinduzi katika
utafiti,uanzishwaji wa mashamba darasa kwa wahitimu wa masomo ya kilimo
na kujenga maabara ya kisasa ya kupima ubora wa mazao yakiwemo mboga
mboga na matunda kabla ya kusafirisha nje ya nchi ili kuongeza thamani
ya bidhaa za kilimo.
Pia
uhamasishaji matumizi ya teknolojia ya bora ya uzalishaji kwa kutumia
zana za kisasa na utoaji huduma za ugani na mafunzo ya muda mfupi kwa
wataalam wa wizara na wakulima kwa kutumia vyombo vya habari na TEHAMA
Ili kuwa na kilimo chenye tija na manufaa kwa mkulima ,Katibu Mkuu
Kusaya amekiomba chuo cha Sokoine kusaidia jitihada za wizara kudhibiti
visumbufu vya mimea na mazao kama viwavijeshi,ndege waharibifu wa kwerea
kwerea, nzige wa jangwani, panya na magugu yanayoathiri mazao ya
wakulima.
“Tunahitaji
sifa nzuri ya ubora wa mafunzo na wataalam wa chuo kikuu cha Sokoine
iendelee na kuwanufaisha wakulima kuongeza tija na uzalishaji kwa
kudhibiti visumbufu vya mazao yake. “ alisema Kusaya.
Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya kilimo kuwa uzalishaji wa ndani wa mbegu bora umefikiatani 61,703 mwaka 2019
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Prof, Raphael
Chibunda alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea chuo hicho na kuwa
wapo tayari kuanzisha mafunzo maalum ya muda mfupi kwa ajili ya
kufundisha wataalam waliopo kazini na wale wanaopenda kujifunza kilimo
cha kisasa. Prof. Chibunda alisema SUA itaendeleza ushirikiano na Wizara
ya Kilimo kupitia taasisi za utafiti wa Kilimo (TARI) na kampuni ya
mbegu nchini (ASA) na Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu Tanzaia (TOSCI)
kuzalisha mbegu bora za mazao kwa kutumia teknolojia na wataalam waliopo
nchini.
“SUA ina msitu wa wataalam hivyo tunaahidi tutashirikiana na wizara ya kilimo kufanya tafiti za mbegu bora na pia kuzalisha mbegu hizo kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. ” alisitiza Prof.Chibunda.
“SUA ina msitu wa wataalam hivyo tunaahidi tutashirikiana na wizara ya kilimo kufanya tafiti za mbegu bora na pia kuzalisha mbegu hizo kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. ” alisitiza Prof.Chibunda.
Aliongeza kusema kina mkakati wa kuanzisha digrii maalum itakayosaidia kuzalisha wataalam wabobezi kwenye usimamizi wa sekta ya ushirika na kilimo nchini ili kuunga mkono jitahada za serikali kuwa na ushirika imara.
Katika hatua nyingine Prof. Chibunda aliomba Serikali iweke utaratibu wa kuratibu waduka ya pembejeo ili yawe na wataalam waliosomea kilimo na mifugo kwa ajili ya kutoa huduma za ushauri kwa wakulima.
Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo alisema lengo la wizara yake ni kuhakikisha kunakuwepo sera nzuri na mazingira wezeshi ya kufanya kilimo kuwa ajira, uchumi na biashara kwa watanzania walio wengi.
Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bw.Gerald Kusaya akiwa ameshika mche wa nanasi wakati alipokagua
shamba darasa la kufundishia wanafunzi chuo Kikuu cha Sokoine leo mjini
Morogoro.Kushoto ni Bw.Ramadhani Omari Mhadhiri wa mafunzo ya bustani
na wa kwanza kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA Prof.Raphel Chibunda.
(Picha na Habari na Wizara ya Kilimo).
(Picha na Habari na Wizara ya Kilimo).
No comments:
Post a Comment