HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 08, 2020

HALMASHAURI YA MKOA WA TABORA ZATOA MIKOPO YA THAMANI YA BILIONI 1.3 KUTOKA MAPAO YA NDANI

Na Tiganya Vincent

HALMASHAURI za Mkoa wa Tabora hadi sasa zimefanikiwa kutoa mikopo ya shilingi bilioni 1.3 kwa vikundi mbalimbali vya vijana , walemavu na wanawake.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ndio inaongoza kwa kutoa shilingi milioni 369 ikiwa ni sawa na asilimia 165 ya makusanyo yake ya ndani na Igunga ilitoa mikopo ya shilingi milioni 180 ikiwa ni asilimia 150 ya mapato yake ya ndani.

Makungu alisema Halmashauri ya Urambo ilitoa mikopo ya shilingi milioni 160 ikiwa ni asilimia 139 , Manispaa ya Tabora ilitoa mikopo ya shilingi milioni 235 sawa na asilimia 132 na Uyui ilitoa mikopo ya shilingi milioni 167 sawa na asilimia 109.

Alitaja Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ilitoa mikopo ya shilingi milioni 66.2 sawa na asilimia 102 , Nzega Mji ilitoa mikopo ya shilingi milioni 90 sawa na asilimia 10 na Sikonge ilitoa mikopo ya shilingi milioni 125 sawa na asilimia 81.

Katibu Tawala huyo wa Mkoa alizitaka Halmashauri kuhakikisha zinafuatilia vikundi vyote vilivyopata mikopo kwa ajili ya kurejesha ili ziweze kusaidia vikundi vingine katika shughuli za maendeleo.
Alisema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kuna jumla ya shilingi milioni 510.7 ambazo zilikopeshwa kwa vikundi vya wanawake , vijana na walemavu hazijareshwa.

No comments:

Post a Comment

Pages