Kampuni ya Kimataifa ya Magari ya TATA
Africa Holding Ltd imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul
Makonda Gari Moja kati ya mbili walizoahidi kumpatia kama sehemu ya
Mchango katika mapambano dhidi ya Corona katika Mkoa huo.
Gari
hiyo aina ya XENON X2 Double Cabin RC Makonda ameelekeza itumike
kuwasafirisha Watumishi wa Afya wanaofanya kazi ya Mapambano dhidi ya
Corona.
Aidha RC Makonda
ameishukuru kampuni hiyo kwa mchango walioutoa na kusema Gari hiyo
itaenda kutatua changamoto za usafiri zilizokuwa zikiwakabili watumishi
wa Sekta ya Afya huku akieleza kuwa hali ya Maambukizi ya Corona katika
Mkoa huo imepungua na Wagonjwa wengi wanazidi kupona.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya TATA Motors, Bwana Rajiv Bhushan
amesema kwa siku ya leo wamekabidhi Gari moja ambapo Gari ya pili
wataikabidhi muda wowote kuanzia sasa.
Aidha
Bw.Rajiv amesema Kampuni hiyo imeona ni vyema ikawa sehemu ya mchango
kwa jamii katika mapambano dhidi ya Corona kwa kuhakikisha watoa huduma
wa Afya wanakuwa na usafiri wa uhakika.
No comments:
Post a Comment