HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 08, 2020

MWILI WA KICHANGA WAOPOLEWA KATIKA MTO KANONI MKOANI KAGERA


Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera,  Hamis Dawa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo .


Lydia Lugakila, Kagera

Wakazi wa mtaa wa Buyekera Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameshuhudia tukio la kinyama baada ya mwili wa kichanga kuonekana ukielea katika mto Kanoni.

Wakizungumzia tukio hilo la kinyama mashuhuda hao akiwemo Angelo John na Adieth Rajab wote wakazi  mtaa wa Buyekera wamesema kuwa wakiwa wanapita katika eneo hilo lenye daraja wameona mwili wa kichanga hicho ambacho kilikuwa kimeishapoteza maisha na kuelea juu ya maji.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Buyekera lilipotokea tukio hilo, Justinian Kamugisha, amesikitishwa na kitendo hicho na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika pindi wanapobaini watu wanaohusika na vitendo hivyo.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kagera, Hamis Dawa, amesema kuwa wamepata taarifa kutoka kwa wananchi juu ya kuonekana kwa kichanga hicho kulazimika kwenda kuopoa mwili huo na kuwa baada ya kuupoa umepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo wakazi hao wamelaani tukio hilo huku wakiomba uchunguzi ufanyike ili kumbaini aliyehusika na unyama huo.

No comments:

Post a Comment

Pages