Na Tiganya Vincent
HALMASHAURI ambazo zinazotegemea
sehemu ya mapato kutoka kwenye zao la tumbaku zimeakiwa kuandaa mkakati mpya
ambao utawawezesha kulima mazao mengine ili kuwa na msingi wa vyanzo vipya vya
mapato ya ndani.
Hatua hiyo inafuatia
Kampuni zinazonunua tumbaku Mkoani Tabora kuendelea kushusha makisio ya
uzalishaji kwa wakulima wa tumbaku.
Kauli hiyo imetolewa jana
na Katibu Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa kikao cha robo ya tatu cha
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Urambo.
Alisema Kampuni za
Tumbaku zimekuja ya staili mpya ya kudai kuwa zitanunua tumbaku kilo chache
lakini badala yake zimekuwa zikinunua tumbaku nyingi iliyolimwa nje ya mkataba
kwa bei inamuumiza mkulima na kusababisha Halmashauri kupata mapato kidogo.
Aidha Makungu alisema ni
vema Halmashauri zikaanzisha kilimo kikubwa cha maembe kwa kuwa Mfanyabiashara
Bakharesa ameshaonyesha nia ya kununua embe zote zinazozalishwa Mkoani Tabora.
Alisema cha msingi
kuwaelimisha wakulima kulima kitaalamu na kutoa huduma za ugani kwao ili waweze
kuzalisha maembe bora.
Makungu aliongeza ni vema
Halmashauri zikasisitiza kilimo cha korosho na Alizeti kwa ajili ya kuwawezesha
wakulima kuwa na vyanzo vingi vya kujipatia kipato.
No comments:
Post a Comment