HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 07, 2020

TMA YATOA TAHADHARI YA MVUA BUKOBA


Na Lydia Lugakila, Bukoba
Kutokana na baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Kagera kukumbwa na mafuriko na kusababisha baadhi ya kaya kukosa hifadhi wakazi hao wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ili kuepuka kukumbwa na madhara zaidi yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa mkoani Kagera, Stephen Malundo, na kudai kuwa kutokana na utabiri uliotolewa inatarajiwa mvua kuwa nyingi katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Mei huku ikitarajiwa kupungua kidogo katika wiki ya tatu na ya nne, na kusisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka manispaa ya Bukoba mkoani kagera wamezitaka mamlaka zinazohusika kuendelea kuchunguza sababu ya ziwa hilo kujaa na kusababisha maji kuingia katika makazi ya watu huku wakiwasihi wananchi kuacha tabia ya kujenga nyumba  karibu na vyanzo vya maji.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa mvua zinazoendelea  mkoani Kagera zimesababisha mafuriko  katika wilaya ya Missenyi na manispaa ya Bukoba.

No comments:

Post a Comment

Pages