Na Lydia Lugakila, Bukoba
Kutokana na baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Kagera kukumbwa na mafuriko na kusababisha baadhi ya kaya kukosa
hifadhi wakazi hao wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ili kuepuka kukumbwa
na madhara zaidi yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa mkoani Kagera, Stephen Malundo, na kudai kuwa kutokana
na utabiri uliotolewa inatarajiwa mvua kuwa nyingi katika wiki ya kwanza na ya
pili ya mwezi Mei huku ikitarajiwa kupungua kidogo katika wiki ya tatu na
ya nne, na kusisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi
kutoka manispaa ya Bukoba mkoani
kagera wamezitaka mamlaka zinazohusika kuendelea kuchunguza sababu ya ziwa hilo
kujaa na kusababisha maji kuingia katika makazi ya watu huku wakiwasihi
wananchi kuacha tabia ya kujenga nyumba karibu na vyanzo vya maji.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa mvua
zinazoendelea mkoani Kagera
zimesababisha mafuriko katika wilaya ya
Missenyi na manispaa ya Bukoba.
No comments:
Post a Comment