Sehemu ya mbele ya Gari hilo kama lilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha.
Ahmad Mahmoud, Arusha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha baada ya
kupata taarifa fiche limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa ujambazi
akiwemo Mganga wa Kienyeji wakiwa na silaha mbili za moto kwa ajili ya
kufanya matukio ya kiuhalifu mkoani hapa.
Akizungumza na vyombo vya habari mkoani hapa Kamanda wa Polisi, Jonathan Shana, amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa ambao ni Steven Godfrey (32) mkazi wa Tabata, Yunusi Hamed (37)mkazi
wa Tanga, Said Hamisi(38) mkoa Dar es Salaam na mwingine Msafiri Yohana (22)
mkazi wa mwanza.
Mnamo tarehe 6 mwezi wa tano mwaka huu majira
ya saa nne usiku huku maeneo ya daraja la Nduruma Kata ya Baraa Halmashauri ya
jiji la Arusha jeshi letu lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa Ujambazi
waliokutwa na bunduki moja na Bastola moja zenye jumla ya Risasi 12 .
Alisema mnamo majira ya saa nne baada ya
kupata taarifa fiche waliweka mtego maeneo ya daraja la mto turuma ndipo
tulipowaona watuhumiwa hao waliotekea Dar es salaam kuja Arusha kwa kutumia
gari aina ya Toyota Crown, lenye namba la usajiri T. 777 DSJ ndipo
walipolisimamisha gari hilo lakini walikaidi amri.
Hata hivyo askari walichukua uamuzi wa
kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwataadharisha lakini waliendelea kukaidi
amri hiyo, ndipo Askari walipoamua kufyatua risasi kwa kulenga matairi ya gari
hilo hali iliyosababisha kufanikisha ukamataji wa watuhumiwa hao huku mmoja wao
aitwaye Msafiri Yohana akiwa amejeruhiwa kwa risasi katika viganja vyake vya
mikono.
Aidha kwa mujibu wa Kamanda Shana katika upekuzi
wa gari hilo kulikutwa na aina za silaha mbili Shortgun (1) na bastola 1
zenye risasi nne za bunduki aina ya Shortgun na risasi nane za bastola
zilizokuwa kwenye magazine pamoja na mikasi mitatu ya kukatia vyuma, nondo
mbili, gundi na madawa mbalimbali ya mitishamba.
Alieleza Kamanda katika mahojiano na
watuhumiwa hao wamekiri kuja Arusha kwa leongo la kufanya uhalifu na watuhumiwa
hao watafikishwa mahakani pindi upelelezi utakapokamilika, ambapo akatoa wito
kwa watu wote wenye nia ya kufanya uhalifu awatafanikiwa kuingia lakini
watatoka majivu.
Pia niwaombe wananchi waendelee kutoa taarifa
sahihi za uhalifu na wahalifu kwa jeshi hilo ili waweze kuzifanyia kazi hali
itakayosaidia kuimarisha utulivu, amani na usalama tulivu uliyopo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha
alilipongeza jeshi hilo kwa kufanya kazi zake kwa weledi na kuwataka wananchi
kufuata Maelekezo ya kutii sheria bila shuruti na wanaoshindwa mmekuwa
mkiwashurutisha kama hawa
Alisema kuwa kila wakati jeshi hilo limekuwa
likiwataka wananchi kutiii sheria bila shuruti na wanaokaidi mmekuwa
mkiwashurutisha leo mmeonyesha mfano mmekamata majambazi wametii sheria na
hawakuuwawa na matokeo yake ni tofauti na huko nyuma wengi walikuwa wakikaidi
na kujikuta wakiuwawa.
|
No comments:
Post a Comment