Muonekano wa Uwanja wa Sokoine.
Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
BAADA ya Rais Dk. John Magufuli kusema anafikiria
kuruhusu kuendelea kwa shughuli za michezo nchini, wamiliki wa uwanja wa
kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya wameanza
kusafisha uwanja huo ikiwa ni maandalizi ya kutumika kwa michezo ya ligi
kuu Tanzania bara na igi daraja la kwanza.
Baada ya serikali kuzuia shughuli za michezo kwa
lengo la kuepusha msongamano ikiwa ni tahadhari ya maambukizi ya virusi vya
corona, viwanja vingi vya michezo nchini vilitelekezwa bila matunzo.
Meneja wa Uwanja Kumbukumbu ya Sokoine Modesutus
Mwaluka alisemam baada baada ya Rais Dk. John Magufuli kutamka kuwa anafikiria
kurejesha shughuli za michezo, kauli hiyo imezindua na ndiyo maana wameanza
kuufanyia marekebisho ikiwemo kufyeka nyasi na kuweka alama.
‘Kauli ya Rais Magufuli imetukumbusha kuwa tunapaswa
kuwa tayari wakati wote na ndiyo maana tumeamua kuanza zoezi ya kufyeka nyasi
na kuweka alama’ alisema Mwaluka.
Baadhi ya wadau wa michezo Jijini Mbeya Yohana
Nazareth na Venance Siulanga waliipongeza hatua na Wamiliki wa Uwanja kuamua
kufanya maandalizi na kutaka wasimamizi na wamiliki wa viwanja vingine vyote
vya michezo nchini kuiga mfano huo.
‘Kiukweli sasa uamuzi ulifanywa na wamilikia wa
Uwanja wa Sokoine ni wakuigwa na wasaimamizi na wamiliki wengine wa viwanja
kuendelea kuvitengeneza mana huenda kauli ya Mh Rais Magufuli ikatekelezwa muda
wowote” alisema Siulang.
Uwanja wa kumbukumbu ya sokoine uliopo jijini mbeya,
unatumiwa kama uwanja wa nyumbali wa
timu za ligi daraja la pili za Tukuyu stars,ligi daraja la kwanza Mbeya
Kwanza,na Boma Fc na timu za ligu kuu ni Mbeya city na Tanzania Prisons.
No comments:
Post a Comment