HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2020

Shahidi aeleza jinsi alivyopeleka sampuli za vielelezo kesi ya kina Shamimu

Na Janeth Jovin

OFISA kutoka Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Juma Suleiman, ameieleza Mahakama Kuu kitengo cha Makosa ya Uhujumu Uchumi kuwa yeye ndiye alipeleka sampuli za vielelezo vya kesi inayomkabili Shamimu Mwasha na Mmewe, katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Abdul Nsembo.

Suleimani alieleza hayo jana wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo mbele ya Jaji Elinaza Luvanda.

Akiongozwa na wakili wa serikali Costantine Kakula, Suleiman alidai Mei 2 mwaka 2019 alikabidhiwa vielelezo hivyo na Ispekta Johari pamoja na fomu ya uwasilishaji wa sampuli katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikaki.

Alidai, sampuli hizo zilipokelewa na mkemia aliyemtaja kwa jina la Fidelis Segumbo kwa ajili ya uchunguzi, saa 8 mchana na kusajiliwa.

"vielelezo hivyo vilikuwa ni bahasha tano, katika uchunguzi wa awali mkemia alibaini kuwa baadhi ya vielelezo hivyo ni dawa za kulevya akna ya Heroin, kisha alivifunga kwa lakili ya mkemia, aligonga mhuri n akuweka sahihi yake" alidai Suleiman

Alidai, baada ya uchunguzi vielelezo hivyo ambavyo vilikuwa ndani ya bahasaha A, B, C, D, E, alivirudisha ofisi z DCEA na kumkabidhi Johari.

Katika kesi hiyo,Shamimu ambaye ni mmiliki wa Blog 8020 Fashion na mumewe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye shtaka la  kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70

Washitakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Mei 13, mwaka jana.

Inadaiwa Mei Mosi, mwaka jana wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, washitakiwa walisafirisha dawa hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages