July 14, 2020

BENKI YA CRDB YAJIKITA KUWASAIDIA WAKULIMA

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali, akimkabidi tuzo ya mdhamini wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataiafa (DITF), Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB,  Stephen Adili, wakati wa kufunga maonesho hayo Juali 13, 20202. (Picha na Francis Dande).
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB,  Stephen Adili, akipokea tuzo ya mdhamini wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB,  Stephen Adili, akiwa ameshika tuzo ya mdhamini katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
 Wadhamini wa maonesho hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali, akizungumza jambo na Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Badru Idd, mara baada ya kufunga Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali, akizungumza jambo na Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Badru Idd, mara baada ya kufunga Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Badru Idd (kushoto), akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Prof. Riziki Shemdoe, katika hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
 
Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Badru Idd (kushoto), akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Prof. Riziki Shemdoe, katika hafla ya kufunga Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Badru Idd, akiteta jambo na  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Prof. Riziki Shemdoe.  Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB,  Stephen Adili.
 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB,  Stephen Adili, akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Prof. Riziki Shemdoe.
 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB,  Stephen Adili,, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Prof. Riziki Shemdoe.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili, akimshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Prof. Riziki Shemdoe. Katikati ni Meneja wa Kanda wa Benki ya CRDB, Badru Idd.
 Picha ya kumbukumbu.
 Picha ya kumbukumbu.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Temeke jijini Dar es Salaam, Andrew Augustine, akiwa ameshika tuzo ya mdhamini katika Monesho ya Sabasaba.
 Tuzo ya mdhamini wa mtoa huduma za kibenki.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Temeke, Andrew Augustine (kushoto), akiwa na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Sabasaba.


Na Francis Dande

Benki ya CRDB inashiriki kikamilifu katika kuhakikisha sekta binafsi inaenda juu zaidi na kuhakikisha wakulima wanapata mikopo katika sehemu zote ambazo wanafanyakazi.

Benki hiyo imejizatiti katika kuhakikisha wakulima wanapata mikopo katika katika sehemu zote ambazo wanafanyakazi na ukiangalia katika mnyororo wa thamani kuanzia mkulima, mtu anayenunua mziko, mtu anayeenda kuchakata kupata kitu na mpaka mtu wa mwisho anayeenda kuuza.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB,
Stephen Adili, wakati wa kufungwa rasmi Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ‘DITF’ jijini Dar es Salaam Julai 13, 2020.

Katika kuelekea uchumi wa juu benki hiyo imesema kuwa itahakikisha inawasaidia watanzania na serikali kwa ujumla kwa kuwa maana tumeshakuwa uchumi wa kati.” Alisema Adili.

“Sisi kama benki tunashiriki kikamilifu katika kuhakikisha sekta binafsi inaenda juu zaidi kwa kutoa mikopo kwa ajili ya wafanyabiashara, mtu mmoja mmoja kupitia idara ya wafanyabiashara wadogowadogo, mama lishe, bodaboda na ya kati ambayo inasaidia wafanyabiashara wadogo kuwa wafanyabiashara wa kati na baadaye kuwa wakubwa.” Alisema Adili.

Benki hiyo imepata tuzo ya mdhamini wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ‘DITF 2020’.

No comments:

Post a Comment

Pages