July 14, 2020

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON ACHUKUA FOMU YA KUWANIA NAFASI YA UBUNGE WA JIMBO LA MBEYA MJINI

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mbeya Mjini, Ndg. Gervas Ndaki wakati alipofika katika ofisi za CCM Wilaya kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) katika ofisi za CCM Wilaya Mkoani Mbeya. Kulia ni Mume wake aliyemsindikiza, Ndg. James Andilile Mwainyekule.
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akitoa hela kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mbeya Mjini, Ndg. Gervas Ndaki tukio lililofanyika leo katika ofisi za CCM Wilaya Mkoani Mbeya.
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akikabidhiwa fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mbeya Mjini, Ndg. Gervas Ndaki tukio lililofanyika leo katika ofisi za CCM Wilaya Mkoani Mbeya. Kulia ni Mume wake aliyemsindikiza, Ndg. James Andilile Mwainyekule. (PICHA NA OFISI YA BUNGE).

No comments:

Post a Comment

Pages