HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2020

DC BUKOBA AMJIA JUU MKURUGENZI MTENDAJI AAGIZA KUUNDWA KAMATI MPYA MATUMIZI YA RDHI

Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Solomon Kimilike kuunda mara moja, kamati ya uchunguzi kutokana na mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kijiji cha Igombe kata ya Nyakato kutofuatwa.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Mkoani
Kagera Deodatus Kinawilo wakati akizungumza na wananchi
katika mkutano wa kijiji uliolenga kutatua mgogoro wa ardhi
uliodumu kwa siku nyingi, katika kijiji cha Igombe kata Nyakato halmashauri ya Bukoba ambapo amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kuunda kamati ya uchunguzi itakayosaidia kujua ni kwa nini mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho haikufuatwa.
 
Kinawilo amesema kuwa kijiji hicho kimekuwa na mgogoro wa ardhi wa siku nyingi huku kukionyesha utaratibu wa mpango wa matumizi bora ya ardhi kutofuatwa. 

Mkuu huyo wa wilaya amesema lengo la serikali kuamua kuleta mpango wa matumizi bora ya ardhi ni kulenga kutatua
migogoro ya ardhi.

Amesema kuwa mpango huo unapitishwa na kijiji kizima na ni shirikishi na baada ya mpango kupitishwa na kusajiliwa
inateuliwa kamati ya kusimamia huo mpango na kamati hiyo
inakuwa na mwenyekiti na katibu na ni kamati ambayo
inahakikisha huo mpango haurubuniwi.

Katika hatua hiyo mkuu wa wilaya amemtaka mkurugenzi huyo kuunda kamati ya uchunguzi wa kujua imekuwaje mpango huo wa ardhi haukufuatwa, huku akimuelekeza kuhusisha afisa usalama wa taifa, takukuru, ikiwemo muhusika toka jeshi la polisi katika kamati hiyo itakayoundwa.
 
Hata hivyo kinawilo amewataka wananchi katani humo kufanya kazi ili kukuza pato la taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages