July 08, 2020

Dk. Abbas asema serikali haina haja ya kutegemea misaada ya nje

Na Tatu Mohamed

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas amesema kuwa serikali haina haja ya kutegemea misaada kutoka nchi za nje wakati nchi ipo kwenye uchumi wa kati.

Dk. Abbas ambaye pia ni Msemaji wa serikali ameyasema hayo leo Julai 7, 2020 wakati alipotembelea maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ’sabasaba’ yaliyo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema Tanzania ina rasilimali nyingi lakini ilikaa muda mrefu kwenye umaskini na kubainisha kuwa imerudi panapostahili kwa kuelekea mbele kwenye uchumi wa kipato cha kati.

“Si kweli, kuna baadhi ya watu nimeona kwenye mitandao wanasema ukiingia kipato cha kati tutakosa misaada, tutakuwa hatukopesheki …kwanza si lazima tupate misaada yote lakini si kweli,” amesema.

Ameongeza kuwa uchumi wa kipato cha kati ni fursa muhimu kwa kupata wawekezaji wakubwa zaidi. 

“Uchumi wa kipato cha kati ni nchi inakuwa si masikini na si tajiri sana, kwahiyo sisi ni matajiri lakini si matajiri sana tunaambana kwenda lakini si masikini,” amesema.

Amefafanua, uchumi wa kipato cha kati ni nafasi nyingine kwa watanzania kutafakari tulipotoka tulipo na tunapopaswa kwenda huku akiwataka wananchi kupenda kufanya kazi kwa ubora, kuwa waadilifu.

“Kama kwenye biashara yako basi uzalishe bidhaa ambazo zenye ubora usitengeneze kidogo ukachomekea ukaharibu, kwani kwenye uchumi wa kipato cha kati unaamika duniani wanaona hospitali zako ni nzuri kwasababu hawakauchukilii kama nchi masikini bali ya uchumi wa kati,” amesema.

Aliongeza kuwa wawekezaji wanapoingia nchini wanakuwa na Amani kuwa bidhaa zinazopatikana nchini ni nzuri kuhu akiwataka wananchi kufanya kazi na kuzalisha zaidi.

“Watumishi wa umma tuwe waaminifu zaidi, hauwezi kuingia kipato cha kati unaamka saa nne, kijana hujisomei vizuri vyuoni, unafanya kazi unaangalia saa muda wote …utakuwa nyuma,”alisema.

Dk. Abbas amesema sekta ya viwanda imeongezeka ambapo tangu uhuru kulikuwa na viwanda vikubwa, vidogo na vya kati vilikuwa 5200 huku miaka minne vipo viwanda zaidi 8000.

“Viwanda hivyo vinazalisha malighafi mbalimbali uwekezaji umechangia, kila mtanzani ukiacha wachache ambao walikuwa walikuwa wakitukana tu.

“Hawajachangia lakini waliojitoa na kufanya kazi kwa bidii walijituma wamejituma lakini kama ulikuwa mzandiki, kuandamana tu kila ukimaka unatafuta figusu haujaingia kipato cha kati,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages