July 08, 2020

MAMIA YA WANANCHI WAJITOKEZA KWENYE MAONESHO YA SABASABA


Na Janeth Jovin

MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoani wamejitokeza katika viwanja vya maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba ) ikiwa ni kusherehekea sikukuu ya sabasaba huku watu wengi wakimiminika katika mabanda ya wasanii na Banda la Maliasili.

Maonyesho ya kimataifa ya sabasaba hufanyika kila mwaka hapa nchini na kushirikisha washiriki mbalimbali kutoka nje ya nchi na katika maonyesho ya Mwaka huu yaliweza kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Licha ya kuwepo kwa foleni kubwa ya kuingia ndani lakini bado utulivu na usalama uliendelea kuwepo katika viwanja vya sabasaba ambapo mbali na wananchi kukimbilia kwenye mabanda ya wasanii kuona wasanii na katika eneo la kuona wanyama .

Watu wamekuwa na maoni mbali mbali ikiwemo mabanda ambayo watu wanakuwa wengi wanatakiwa kuwekwa katika eneo la uwazi.

"Banda kama la wasanii watu ni wengi sana wamefulika kupita kiasi eneo lenyewe lililotengwa ni dogo hivyo mamlaka ingefanya utaratibu wa kuyaongezea ukubwa," alisema Juma Saidi na kuongeza

"Kwenye banda la wanyama napo watu wamejaa hadi mlango umefungwa miaka mingine TanTrade wapange vizuri haya maeneo kwani wanajua watu wengi wanapenda kuingia katika mabanda haya," alisema

Akitembelea Mabanda mbalimbali Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas alisema kwa muda mfupi ambao maandalizi ya sabasaba yalifanyika na kile kilichoonekana leo (Jana) ni ushindi tosha. 

“Nikikumbuka mida ambao tuliruhusu Tantrade iendelee na sabasaba ni mfupi sana, tunawapongeza wadau wote na waandaji kwa sababu wakati tunatangaza ile sabasaba nilikuwa nasema sijui itakuwaje mwaka huu ,"alisema na kuongeza

"Tunaweza kuandika historia ya sabasaba iliyopooza kuliko zote lakini nilipozunguka  nimeona mambo yamefanyika na tofauti nilivyofikiria," alisema

Alisema mabanda mengi yapo wazi sababu ya wafanyabiashara wa nje kuogopa corona ila watanzania wamejitokeza kwa wingi katika kujionea vitu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages