July 17, 2020

GOBA ROADS RUNNERS CLUB YAANDIKA HISTORIA KWA KUANDAA TUKIO LA MBIO NDEFU ZAIDI TANZANIA

Washiriki wa mbio za Dar-Moro Run wakichuana katika mbio hizo zilizoanzia jijini Dar es Salaam na kuishia Morogoro.
 Washiriki wa mbio za Dar-Moro Run wakichuana katika mbio hizo zilizoanzia jijini Dar es Salaam na kuishia mkoani Morogoro.
 Washiriki wa mbio za Dar-Moro Run wakichuana katika mbio hizo zilizoanzia jijini Dar es Salaam na kuishia mkoani Morogoro.
Ofisa michezo Mkoa wa Morogoro, Grace, akimkabidhi cheti mwakilishi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.
Ofisa Michezo Manispaa ya Ubungo (kushoto), akimkabidhi tuzo Mhandisi Patrick Katemba.






Goba Roads Runners (GRR) ni Klabu wa wakimbiaji yenye maskani yake katika viunga vya Goba Jijini Dar es salaam. Wanachama wa klabu ni wakazi wa sehemu mbali mbali katika wilaya zote za Jiji la Dar Es Salaam na wa nje ya Dar Es Salaam.

Katika klabu yetu tuna mafunzo mbalimbali katika ngazi tofauti za wakimbiaji.

Tuna wale wanaoanza yaani (Beginners), kuna wenye uwezo wa kati yaani (Intermediate), Wenye uwezo wa mbio ndefu au long run na ultra long run (advanced).

Tukio hili ilikuwa ni sehemu ya mafunzo kwa mbio ndefu yaani Ultra Run, na kwa kuwa Klabu ina malengo ya kuendesha Ultra Marathon Juni, 2021, mbio hii imetumika kama maandalizi.

Mafunzo haya yamehusisha wakimbiaji toka GRR na klabu nyingine kama vile Moro Runners Club, Kigamboni Amsha Amsha Club na  Wasafi Jogging Club.

Tulipata hamasa kubwa kutoka kwa Moro Runners waliotupokea kutoka Mikese mpaka Morogoro Mjini.

Mbio hii imeleta hamasa kubwa miongoni mwetu na kudumisha mahusiano  mazuri baina yetu. 

Tunawashukuru sana wanachama wa klabu waliochangia kufanikisha mbio hii, wanachama walioshiriki katika kutoa huduma mwanzo hadi mwisho wa mbio, wadhamini mbali mbali waliotoa michango yao, Jeshi la Polisi Tanzania, Viongozi wote wa michezo Wilaya ya Ubungo inapotokea klabu, Viongozi wa Michezo mkoa wa Morogoro na wilaya zake, Chama cha Riadha Taifa na Baraza la Michezo Taifa waliohakikisha zoezi hili linaenda ilivyotarajiwa.Waliofika Morogoro walikuwa ni Edson Mwakalukwa, Eng. Patrick Katemba, Joseph Katembo na Bakari Semeng'anda..Hawa walitumia Masaa 19:35:25

Wanawake walikimbia umbali tofauti ambapo  aliyekwenda umbali mrefu zaidi alienda hadi Mdaula, umbali wa km 120, kwa masaa 16:25:31. Jina Arafa Msalo.

Wengine ni Mariam Mwalim aliyekimbia km 108 na Janeth Mtenga alieenda km 105.

pia kulikuwa na mlemavu wa viungo aitwaje Shukuru Halfan ambaye alikimbia Kilometa 155 kwa muda wa saa 17:20:00.

Wengine walioshiriki kati ya umbali wa kilometa 100 hadi 150 ni 

Karim Chang'a, Alfred Malanji, Baraka Konkara, Johnson Mbunda, William Mutahangarwa, 
Proches Julius,  Benson Luaga, Joshua Kayombo, Modibo Coulibaly, Lister Pakua, Dawson David, Abbas Adam,

1 comment:

Pages